Wanaharakati Kenya wataka watenda ghasia za 2008 kuhukumiwa

...................

Mfuasi wa chama cha Orange Democratic Party  ODM akibepa panga mbele ya kizuizi kinachowake moto wakati wa ghasia za 2008 katika kitongoji cha Kibera Nairobi.
Mfuasi wa chama cha Orange Democratic Party ODM akibepa panga mbele ya kizuizi kinachowake moto wakati wa ghasia za 2008 katika kitongoji cha Kibera Nairobi.

Mungano wa vyama vya kutetea haki za kiraia unaojulikana kama Wakenya kwa ajili ya Amani wenye Ukweli na Haki, KPTJ, kimezindua ripoti iliyopewa jina la "Securing Justice."

Ripoti hiyo inatoa wito kwa serikali ya Kenya kuunda mahakama maalum kuwahukumu wale walohusika moja kwa moja katika kushambulia watu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi 2008.

Akizungumza mjini Nairobi wakati wa kuzindua ripoti, mratibu wa KPTJ, Bi, Carole Theuri, alisema kunahaja ya kuundwa mahakama itakayowahukumu wale watu wa kawaida walotenda ghasia za 2008.


Kutoka VOA http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: