CCM IMEDHAMIRIA KUshinda kaTA ZOTE 25
NA BASHIR NKOROMO, IRINGA
CHAMA Cha
Mapindizi (CCM) kimesema kimedhamiria kushinda kwenye kata zote 25
katika uchaguzi mdogo wa madiwani ambao kampeni zake zinaendelea katika
kata mbalimbali nchini.
Hayo
yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati
akizungumza na wananchi katika kata ya Mbalamaziwa, wilayani Mufindi
mkoani Iringa, ambako zinaendelea kampeni za udiwani katika kata hiyo.
Katika Kata hiyo bendera ya CCM inapeperushwa na Zuberi Nyamoleo.
"Kutokana
na jeshi kubwa na wafuasi tulio nao na imani inayoendelea kuonyeshwa na
wananchi kuiunga mkono CCM, tuna imani dhamira hii itafanikiwa bila
shaka yoyote", alisema Kinana na kuongeza;
"Pale
Mbinga katika Kata ya Lokindo CCM imeshapita bila kupigwa, wapinzani
wenyewe wametuachia kwa sababu wameridhika kuwa tunafaa kiuwaongoza, na
pele Iramba Vijijini, Chadema walijaribu kuchacharika lakini wameambulia
matupu vijiji vinane vyote vimeenda CCM".
Kinana
aliwapongeza wagombea wengine waliokuwa katika mhakato na Nyamoleo kwa
kuamua kuuga mkono mgombea wa CCM katika 'vita' hiyo ya kuwania udiwani
katika kata ya Mbalamaziwa.
"Ninyi ni
watu wa kuheshimika sana ndani ya CCM, mmefanya uamuzi wa busara kuamua
kumsaidia mgombea wa CCM aliyejipita kwenye kura za maoni. Huu ndiyo
ustaarabu na moyo wa dhati unaotakiwa kwa kila mwana-CCM", alisema
Kinana.
Kinana
alisema, wanachama walio bora ndani ya CCM ni wale wasio na ubinafsi kwa
kung'ang'ania kila wanachotaka wapate na wanapokosa inakowa nongwa.
"Mwanachama
lazima uelewe kwamba unapogombea nafasi yoyote inayowaniwa na wengi
huwa kuna kushinda au kushindwa, sasa inapotokea umeshindwa ni lazima
uendelee kuwa mwaminifu kwa chama ili kuhakikisha kinashinda", alisema.
Kinana
alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kutwaa kata zote, lazima
wagombea watakaposhinda wawe watumishi wenye kujinyenyekeza kwa wananchi
siyo kujinyayua mabega kana kwamba wao ndiyo bora kuliko wanaowaongoza.
"Tafadhalini
sana, Chama hiki ni cha wananchi, diwani atakayeshinda ahakikishe
ushindi aliopata haugeuzi kuwa utukufu kwake kabla ya utumishi, huyo
tutamshughulikia mara moja", alisema Kinana.
Kinana
alipita katika kata hiyo akiwa njiani kwenda wilayani Njombe ambako
anaanza ziara ya siku saba akifuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye.
mwisho.
kupitia mtandao-net
0 comments: