Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

HARUFU YA VITA KATI YA MAREKANI NA KOREA HII HAPA

0 comments

Kwa muda mrefu kumekuwa na hali ya kurushiana Maneno kati ya marekani na N. Korea, hali hiyo imeleta sintofahamu baada ya vitendo vinavyoendelea. N. Korea imefanya tamasha la kijeshi LA zana za ulinzi kama tishio LA vita vya kinyuklia na kwa upande wa pili marekani NATO inajiandaa kivyake. Kwa hali hiyo kuna hatari ya kutokea vita kati ya marekani na korea ya Kim
Taifa LA China limeingilia kati kutaka usuluhishi kati ya wababe hao, bado sintofahamu IPO

Taarifa za kina bofya link hii us-war-with-n-korea-may-break-out-any-moment








Read More »

BANGI NDANI YA MCHAKATO WA KURUHUSIWA KENYA

0 comments
Nchini kenya kumetolewa ombi la kuruhusiwa matumizi ya bangi kwa raia. Jambo hili linapata msukumo sababu nchi nyingi duniani zinaruhusu matumizi ya bangi. Kwa nchi ya Kenya watu wapatao 1,400 wamesapoti hili.
Zaidi bofya hapahabari-39586413

Read More »

Ujenzi wa Ikulu ya rais wa Burundi kukamilika mwaka huu

0 comments



Mradi wa ujenzi wa Ikulu ya rais wa Burundi unatarajiwa kukamilika mwaka huu.
Mradi huo utaboresha mazingira ya kikazi ya viongozi wa Burundi, kuchangia maeneleo ya uchumi wa sehemu zilizo karibu na kuwa alama ya taifa hilo.
Mradi huo unaofanywa kwa msaada wa serikali ya China, uko kaskazini mashariki mwa Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, na umetoa nafasi za ajira kwa watu mia tatu nchini humo, ambao wamepewa mafunzo ya kiufundi kwa nusu mwezi na zaidi kabla ya kuanza kazi.
Kansela wa uchumi kwenye ubalozi wa China nchini Burundi Lu Jun amesema, China na nchi za Afrika zinapaswa kutendeana kwa udhati wa moyo, na kwamba China ina uzoefu wa kutosha katika kujiendeleza, na inapenda kusaidia nchi za Afrika kupata maendeleo

Chanzo: http://swahili.cri.cn/

Read More »

HILI LA MADAKTARI KENYA LIFIKIRIWE

0 comments

Madaktari Kenya wakataa nyongeza ya asilimia 40 iliyopendekezwa na Serikali

mediaPicha ikionesha manesi na madaktari wakiwa kwenye mgomo wao kushinikiza Serikali kutekeleza madai yao ya mshahara.REUTERS/Thomas Mukoya
Chama cha madaktari nchini Kenya kimekataa pendekezo lililotolewa na ikulu ya Mombasa kufuatia mkutano wao na rais Uhuru Kenyatta, ambaye alisema Serikali yake iko tayari kuongeza asilimia 40 ya mshahara wa madaktari hao ili wasitishe mgomo.
Hata hivyo kikao kilichoketi Ijumaa ya tarahe 6 jijini Nairobi, katibu mkuu wa chama cha madaktari Ouma Oluga, amewaambia wanahabari kuwa, baada ya kujadiliana wameamua kutokukubali pendekezo la serikali la asilimia 40.
Oluga amesema kuwa pendekezo lililotolewa na rais Kenyatta licha ya kuwa alionesha nia njema ya kutaka kumaliza mgomo unaoendelea, lakini wao hawako tayari kukubaliana na pendekezo hilo na kwamba mgomo wao utaendelea hadi pale Serikali itakapokubali kutekeleza makubaliano yao ya mwaka 2013.
Mwaka 2013, chama cha madaktari na Serikali ya Kenya walitiliana saini makubaliano ya nyongeza ya mshahara ya asilimia 300 kwa madaktari hao, pamoja na kulipwa marupurupu mengine wanayoidai Serikali.
Mmoja wa madaktari ambao wanashiriki mgomo, wakiandamana hivi karibuni jijini Nairobi.REUTERS/Thomas Mukoya
Mwenyekiti wa chama hicho, Samweli Oroko, amesema kwa sasa wako tayari kuendelea na mazungumzo na Serikali ili kupata muafaka na hatimaye kusitisha mgomo wao, lakini akaongeza kuwa hawako tayari kukubaliana na pendekezo la Serikali ambalo wanasema halitamaliza shida zinazowakabili.
Ni zaidi ya mwezi mmoja sasa, toka madaktari nchini Kenya waanze mgomo wa nchi nzima katika hospitali za uma na binafsi, wakishinikiza Serikali kutekeleza makubaliano yao ya mwaka 2013.
Juma moja lililopita, madaktari nchini humo walimtaka rais kama kiongozi wa juu wa nchi, aingilie kati mgomo wao, ombi ambalo hata hivyo rais Kenyatta alilisikiliza na kukubali kukutana nao mwanzoni mwa juma hili ambapo akapendekeza nyongeza ya asilimia 40.
Mgomo huu wa madaktari umesababisha kuzorota kwa huduma za afya nchini Kenya, ambapo maelfu ya wagonjwa wameendelea kuugulia nyumbani wasijue ni wapi pa kupatia matibabu, huku wengine wakiripotiwa kupoteza maisha

Chanzo:http://sw.rfi.fr/eac/20170106

Read More »

UMEIPATA HII YA MAREKANI....?

0 comments

Msomali aapishwa kuwa mbunge Marekani

Ilhan Omar wa chama cha Democrat anakuwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Somalia kuapishwa kuwa mbunge akiliwalikisha jimbo la Minnesota linalokaliwa na Wasomali wengi zaidi Marekani.
Mbunge huyo mwenye umri  wa miaka 34 alianza rasmi kazi yake hiyo jana (Januari 3) mjini Saint Paul.
Ilhan alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka jimbo la Minnesota katika uchaguzi wa Novemba 8, ambao pia ulimuingiza madarakani Donald Trump kuwa rais wa Marekani, huku akiendesha kampeni ya kupinga wageni, na hasa Waislamu.
Mwanamke huyo aliyewahi kuishi kwenye kambi ya wakimbizi nchini Kenya, aliwasili Marekani mwaka 1995, akiwa mtoto pamoja na familia yake wakikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia.
Alianza kuvutiwa na masuala ya siasa akiwa na umri wa miaka 14. Katika jimbo la Minnesota, kunaishi watu 40,000 wenye asili ya Somalia, ikiwa ni idadi kubwa kuliko jimbo jengine lolote nchini  Marekani.


chanzo:dwswahili

Read More »

MJENGO WA HITLER KUTWALIWA NA SERIKALI

0 comments
Bunge nchini Austria limepitisha sheria inayotoa fursa ya kutwaa nyumba ambapo kiongozi wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler alizaliwa mwaka 1889.
Mmiliki wa sasa wa nyumba hiyo Gerlinde Pommer amekataa mara nyingi kuuza nyumba hiyo inayopatikana Braunau am Inn.
Amekataa pia kukubali ifanyiwe ukarabati.
Bi Pommer sasa atalipwa fidia na nyumba yake itwaliwe.
Lakini haijabainika serikali itafanyia nini nyumba hiyo ambayo zamani ilitumiwa kama mgahawa.
Serikali hata hivyo imeonyesha nia ya kutaka kuzuia nyumba hiyo kuwa kivutio kwa watu wanaofuata sera za Wanazi.
Uamuzi huo wa bunge utafikisha kikomo mzozo wa muda mrefu kati ya serikali na Bi Pommer, ambaye kwa sasa amestaafu

zaidi habari hii inapatikana hapa bbc.com/swahili/habari

Read More »

KUTOKA MAGAZETINI LEO 03.12.2016

0 comments



December 3 2016 naanza kukusogezea post zote kubwa kwenye zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye,Udaku, Hardnews na Michezo ili uje kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye Facebook, Twitterna, Instagram @millardayo ili niwe nakutumia kila kinachoonifikia
img_20161203_055339
img_20161203_055403
img_20161203_055415
img_20161203_055432
img_20161203_055457
img_20161203_055509
img_20161203_055520
img_20161203_055531
img_20161203_055548
img_20161203_055600
img_20161203_055615
img_20161203_055656
img_20161203_055715
img_20161203_055726
img_20161203_055752
img_20161203_055810
img_20161203_055835
img_20161203_055849
img_20161203_055907
img_20161203_055920
img_20161203_055931
img_20161203_055944
img_20161203_055957
img_20161203_060010
img_20161203_060020
img_20161203_060034

Read More »

UTABIRI WA FIDEL CASTO ULIVYOTIMIA

0 comments
katika utawala wake, cuba na marekani hawaja wahi elewana. kwa mitazamo na maono yake akawaambia wa cuba kuwa "WAMAREKANI WATAKUJA KUZUNGUMZA NASI WAKATI WATAKAPO KUWA NA RAIS MWENYE ASILI YA AFRICA NA DUNIA ITAKAPO KUWA NA PAPA KUTOKA AMERIKA YA KUSINI

Read More »