Gavana wa chama tawala afurushwa Nigeria
Chama tawala nchini Nigeria
kimemsimamisha uwanachama kwa muda gavana mwenye ushawishi mkubwa nchini
Nigeria, Rotimi Amaechi, ambaye hamuungi mkono Rais Goodluck Jonathan
kuwania tena urais mwaka 2015.
Bwana Amaechi,kutoka jimbo lenye utajiri mkubwa
wa mafuta Rivers state, aliteuliwa mwishoni mwa wiki kuwa mwenyekiti wa
kikao cha magavana kote nchini.Kawaida Magavana wa majimbo 36 ya Nigeria wana ushawishi mkubwa na wametengewa pesa nyingi kwa ajili ya usimamizi wa majimbo yao.
Mwandishi wa BBC mjini Lagos, Will Ross, anasema kuwa magavana wana ushawishi mkubwa kushawishi wapiga kura kumchagua mgombea fulani katika uchaguzi wa kitaifa.
Bwana Amaechi, mwenyekiti wa sasa wa kikao cha magavana kote nchini alipata kura 19 dhidi ya kumi na sita za mpinzani wake wakati akichaguliwa kwa wadhifa huo. Gavana mmoja hakuhudhuria shughuli hiyo.
Bwana Jang,mwanachama wa (PDP), pia alipinga matokeo ya uchaguzi huo.
Wadadisi wanasema kuwa washirika wa rais wanataka kupunguza ushawishi wa gavana huyo.
Katika mkutano wa dharura wa chama hicho, Jumatatu, maafisa walisema kuwa bwana Amaechi amefurushwa chamani kwa muda kwa kukiuka sheria za chama.
kutoka bbcswahili
0 comments: