MAMA NGWEA"MWANANGU ALINIAHIDI KUWA ATARUDI IJUMAA ILIYOPITA".
...................
Marehemu Albert Mangwair enzi za uhai wake.
Akiongea kupitia kipindi cha Amplifire cha Clouds FM, kutoka mkoani
Morogoro, mama mzazi wa msanii Albert Mangwair aliyefariki dunia leo
akiwa nchini Afrika Kusini, amesema kuwa mara ya mwisho kuwasiliana na
marehemu ilikuwa wiki mbili zilizopita ambapo Mangwair alimwambia kuwa
mzima na anaendelea vizuri na kwamba angerejea nchini Ijumaa iliyopita.
Aliongeza kuwa taarifa za kifo cha mwanaye amezipata jioni hii kwa
masikitiko. Wakati Mangwair anaelekea Afrika Kusini hakumuaga mama yake
japo akiwa huko alikuwa anawasiliana naye. Kuhusu taarifa za mazishi
mama Mangwair amesema bado anasubiri shemeji zake wafike ili wapange.
Mungu ampumzishe Mangwair mahali pema peponi. Amen!
GIVE YOUR OPINIONS HERE
0 comments: