ULANGUZI WA WATU BADO UPO?SOMA HAPA...!

...................

Kisa cha ulanguzi wa watu Bangladesh

 

Zaidi ya raia 80 wa Bangladesh inadaiwa kuwa walisafirishwa hadi Brazil na walanguzi wa watu na kuokolewa na poilisi wa eneo la, Brasilia. Walikuwa wamehadaiwa kuwa watakuwa wakipokea mshahara wa dola 1,500 kila mwezi.
Polisi wanasema kuwa waathiriwa hao wamekuwa wakiishi kwa taabu katika viunga vya jiji hilo.
Raia hao wa Bangladesh walikuwa wamesafiri kilomita elfu kumi na sita na kuingizwa Brazil bila pasi za usafiri na waliingilia katika mipaka ya Peru, Bolívia na Guyana.
Walikuwa wamelipa kila mmoja dola 10,000 kwa walaghai waliowahamisha kutoka Bangladesh. Kulingana na gazeti la Estado de São Paulo, ushahidi upo kuonyesha kuwa walikuwa wakinyanyaswa katika miradi wanayoshughulikia ya ujenzi wa nyumba.
Polisi walianza kuwashuku watu hao kutokana na kuongezeka kwa raiya wa Bangaladesh nchini humo wanaoliza hadhi ya ukimbizi.

Na bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: