GONGO NOMA:MKE WA NAIBU CHIFU AFARIKI DUNIA MARA BAADA YA KUNYWA GONGO KUPITA KIASI
MKE
wa naibu wa chifu katika wilaya ya Marigat Alhamisi aliaga dunia katika hali
isioeleweka baada ya mumewe kumpata akinywa pombe haramu ya chang’aa katika
nyumba ya jirani.
Naibu
wa chifu wa kata ya Arabal Bw William Yegon inasemekana hakufurahia pale
alipompata mkewe Bi Mary Kobilo, 46, akipiga mtindi na wanakijiji wengine.
Wenyeji
walioongea na Taifa Leo walisema kuwa wawili hao walianza kuzozana wakati wa
tukio hilo la saa kumi na mbili jioni Jumatano huku naibu huyo wa chifu
akimlaumu mkewe kwa kumwaibisha kwa kunywa pombe hiyo haramu ilhali yeye
alikuwa afisa wa serikali anayefaa kuongoza vita dhidi ya pombe haramu.
“Naibu
huyo wa chifu alikasirishwa sana kwamba mkewe alikuwa akimkosea heshima licha
ya serikali kutangaza vita kwa wapikaji wa pombe haramu,”alisema mmoja wa
wanakijiji ambao hakutaka kutajwa jina.
Alisema
kuwa baada ya ugomvi huo marehemu alipepesuka nje ya nyumba lakini hakwenda
nyumbani kwake. Mwili wake ulipatikana katika msitu mmoja karibu na kwake
Alhamisi mchana.
Akithibitisha
tukio hilo,mkuu wa wilaya ya Marigat Bw Saul Moywaywa alisema kuwa uchunguzi
tayari umeanzishwa kubaini kiini cha kifo cha mwanamke huyo.
Sumu
“Mwili
wake haukuwa na alama yoyote. Tunashuku alijitoa uhai wake kwa kumeza sumu,”Bw
Moywaywa aliambia Taifa Leo kwa njia ya simu.
Mwili
wa marehemu ulichukuliwa na kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya
wilaya ya Kabarnet kusubiri upasuaji
Na gumzo la jiji
0 comments: