Kundi la LRA lajihusisha na biashara ya meno ya tembo.
Caesar Achellam, kamanda wa cheo cha juu wa kundi la LRA
Ripoti mpya imesema kwamba kuna ushahidi mkubwa kuwa kundi la waasi
la (LRA) linajishughulisha na ujangili wa meno ya tembo huko Afrika ya
kati.
Taarifa hiyo iliyotolewa Jumatatu , inasema LRA wanatumia biashara hiyo haramu ya meno ya tembo kama njia ya kujikimu.
Ugunduzi unatoka katika mashirika mawili yenye makazi yake Marekani, mradi wa Enough, na mradi wa satellite Sentinel kulingana na uchunguzi uliofanyika katika hifadhi ya taifa ya wanyama ya Garamba katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Msemaji wa mradi wa Enough Jonathan Hutson hivi karibuni alitembelea hifadhi hiyo. Katika mahojiano na VOA amesema mfungwa wa zamani wa LRA ni mmoja wa wale walioelezea ukatili katika eneo hilo.
Hutson anasema mfungwa huyo anasema ameona wapiganaji wa LRA wakipiga risasi tembo na kukata nyama za maiti ya tembo hao.
Na wanachama wengine wa LRA waliojitoa katika kundi hilo wanaripoti kwa nyakati tofauti waliona helikopta nyeupe zikituwa kwenye mbuga hiyo na kununua pembe za ndovu kwa kuwapa wapiganaji silaha,bunduki na vyakula.
LRA wakati fulani walipambana na serikali ya Uganda lakini kwa sasa wamekuwa ni kikosi cha wapiganaji wanaozunguka zunguka huko Congo, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Na VOA
0 comments: