Rais Banda azindua mpango wa ajira wenye utata
Muimbaji maarufu wa muziki wa kiroho au Gospel nchini Malawi Joseph
Alfazema ameamua kuacha kuazi ya kuimba kwa sasa kwa ajili ya kupata
kibarua cha watu wasiokuwa na utaalamu nchini Korea Kusini
Joseph Alfazema ni miongoni mwa maelfu ya Waamalawi walioamaua kwenada
Koraea kusini kutokana na mpango wenye utata wa ajira ulioanzishwa na
Rais joyce banda, kupamnbana na ukosefu wa ajira katika taiafa hilo
masikini la kusini mwa Afrika, ambalo lina ukosefu wa kazi wa 50
asilimia
wakosoaji lakini wanahofia kwamaba mpango huo unaweaza kugeuka kuawa utumwa mambo leo. Hata hivyo Waziri wa kazi Eunice Makangala amezipuuza hofu hizo akiliambia bunge hivi karibuni kwamba si utumbwa wa kisasa hata kidogo.
Mpango wa rais huyo ni wa kupatia ajira vijana wanaomaliaza shule na ambao hawana la kufanya, ikiwa ni jitihada za kulitafutia ufumbuzi tatizo la ukosefu mkubwa wa kazi nchini Malawi.Hadi vijana 200,000 huingia katika soko la ajira nchini Malawi kila mwaka, ingawa ni nafasi 40,000 tu mpaya za kazi zinazoundwa-ikiwa ni kwa mujibu wa wataalamu wa ajira.
Nchini malawi, ambayo ni miongoni mawa nchi zenye maendeleo duni duniani, kiasi ya 40 asili mia ya watu milioni 13 wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku.
Msaada wa wafadhili ni kiasi ya 40 asili mia ya bajeti ya serikali. Alipoanzisha mpango huo mwezi Machi Banda alisema " Ninataka wakafanye kazi kwa bidii na kuwashangaza Wakorea kusini."
Aidha Malawi inapanga kuwapeleka wafanyakazi wahamiaji hadi 100,000 wenye umri kati ya miaka 19 na 40 huko Korea kusini, Dubai na Kuwait. Serikali sasa imeanzisha utaratibu wa kuzitangaza nafasi za kazi katika sekta ya kilimo na hospitali. Alfazema ni miongoni mwa watu wa kwanza kupata nafasi kama mkulima.
Anasema,"Siiachi kazi yangu ya uwanamuziki, lakini nataka kwenda nikatengeneze pesa niweze kuwa na vifaa vyangu mwenyewe vya muziki."
Wafanyakazi watakaokwenda nchini Korea Kusini hupata msahahara wa hadi Dola 1000 kwa mwezi wakilinganisha na mshahara wa nyumbani wa dola100 kwa mwezi katika taasisi za umma na binafsi.Kuna dalili zinazoonesha kuwa Malawi kugeuka chanzo cha kutumikishwa bila ya kulipwa malipo yanayostahiki.
Wadau wa ajira wahofia mpango huo wa Rais Banda
Kiongozi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali linaloitwa National League for Democracy and Development, Billy Mayaya, anahofia kwamba mpango huo utasababisha kuweko kwa utumwa mambo leo. Nafasi za unyonyaji ni kubwa na badala yake anasema serikali ingejaribu kufungua nafasi za ajira nyumbani-malawi.
Steven Kamwendo Mbunge wa chama tawala cha zamani Democratic Progressive cha Marehemu Bingu wa Mutharika ameionya serikali iwe wazi kuhusu masharti ya kupelekwa wafanyakazi katika nchi hizo, kabla ya kuwapeleka.
Kamwendo alisema " Daima tumekuwa tukipiga kelele juu ya kuwahimiza wamalawi wenye ujuzi na maarifa walioko nchi za nje warudi nyumbani, na sasa tunasafirisha tulionao nyumbani na kuwapeleka wakatumike kama wafanyakazi nje."Alisema haiingia akilini hata kidogo.
Waziri wa kazi bibi Makangala anasema, Malawi si nchi ya kwanza kupeleka wafanayakazi nje, kukiwa na nchi 16 zilizosaini mkataba wa kutuama wafanyakazi wahamiaji mashariki ya kati. Akaongeza, kuna nafasi zaidi za ajira nchini Dubai na Kuwaita kwa kazi za wafanyakazi wenye ujuzi na wa wasio na ujuzi.
Mwandishi: Hashimu Gulana/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
Na dw swahili

0 comments: