Wanajeshi wakabiliana na Tuareg Mali

...................

Tuareg wanataka kujitenga na Mali

Wanajeshi nchini Mali wamekabiliana na kundi linalotaka kujitenga Kaskazini mwa Mali la Tuareg, katika mji wa Kidal, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi.
Mji wa Kidal umekuwa ukidhibitiwa na kundi linalopigania ukombozi wa Azawad (MNLA) tangu mwezi Februari , wakati wapiganaji wa kiisilamu walipoutoroka mji huo.
Kundi la MNLA lilikuwa likishirikiana na makundi mengine ya kiisilamu wakati walipoliteka eneo la Kaskazini mwa Mali mwaka jana.
Lakini makundi hayo yalitawanyika na hata kuunga mkono jeshi la Ufaransa dhidi ya kundi hasimu.
Ni mara ya kwanza kwa jeshi la Mali kupambana na wapiganaji hao, wa Tuareg wanaotaka kujitenga tangu jeshi la ufaransa kuingilia mzozo wa Mali mwezi Januri.
Wadadisi wanasema kuwa jeshi la Mali linataka zaidi kuhakikisha kuwa mji wa Kidal, ambao uko Kaskazini mwa nchi, karibu na mpaka wa Algeria unadhibitiwa na serikali kabla ya uchaguzi wa tarehe 28 mwezi Julai.
Tuareg wamesema kamwe hawataruhusu maafisa wa utawala wa Mali kuingia katika mji wa Kidal kabla ya uchaguzi kufanayika
Zana nzito zilipatikana , alisema msemaji wa jeshi Kanali, Souleymane Maiga, akiongeza kuwa jeshi lilikuwa linapambana na makundi yaliyojihami Kusini Magharibi mwa Kidal karibu na kijiji cha Anefis.
Aliongeza kuwa majeshi yalikuwa yanashika doria wakati yaliposhambuliwa.

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: