...................
Udugu wa kiislamu umeitisha maandamano nchini Misri leo kwa
kughadhabishwa na kung'olewa madarakani na jeshi kwa Rais
Mohammed Mursi na kukamatwa kwa kiongozi wao na maafisa
wengine wakuu.Kuna hofu kuwa kuondolewa madarakani kwa Mursi
huenda kukazua ghasia nchini humo na makundi ya zamani ya
wapiganaji wenye itikadi kali yameapa kupigana.Wapiganaji wa
kiislamu wanashukiwa kuyashambulia maeneo manne kaskazini
mwa Sinai wakilenga vituo viwili vya ukaguzi vya kijeshi,kituo cha
polisi na uwanja wa ndege wa el Arish ambako kuna ndege za
kijeshi.Mwanajeshi mmoja aliuawa na wengine watatu kujeruhiwa
kulingana na maafisa wa usalama ambao hawakutaka majina yao
kutajwa kwasababu hawana ruhusa ya kuzungumza na
wanahabari.Chama hicho kilipigwa marufuku kwa miaka mingi nchini
Misri hadi alipong'olewa madarakani Rais Husni Mubarak. Mursi
ndiye Rais wa kwanza kuchaguliwa na wamsri kutoka chama cha
udugu wa kiislamu.Uchaguzi huo pia ulikuwa wa kwanza wa
kidemokrasia nchini humo.
chanzo:dwswahili
GIVE YOUR OPINIONS HERE
0 comments: