ZITTO: CHADEMA, NCCR MAGEUZI KUONGOZA HALMASHAURI YA UVINZA
CHADEMA
na NCCR-MAGEUZI tuna jumla ya madiwani 13 katika Halmashauri ya Wilaya
Uvinza. Ni mamlaka mpya inaanza tarehe 20 Julai, 2013. CCM ina madiwani nane
tu, hivyo a clear majority kwa upinzani. CHADEMA ina madiwani saba, NCCR-MAGEUZI watano + Mbunge mmoja.
Leo sekretariat za vyama vyetu zinakaa kuamua chama gani kati ya CHADEMA na NCCR-M kitoe Mwenyekiti, makamu na wenyeviti wa Kamati.
Nimewaambia madiwani wetu kwamba Ni
lazima kuhakikisha Halmashauri hii inaongozwa na Upinzani. Tukiendekeza
tamaa zetu za kisiasa CCM watapita katikati yetu. CCM wakichukua
Halmashauri ya Uvinza yenye madiwani wengi wa upinzani itakuwa ni
usaliti mkubwa kwa wananchi.
Nimewasihi viongozi wa vyama vyote viwili kuwa
na hekima na kuzingatia matakwa ya wananchi waliotoa ridhaa mwaka 2010
na hivyo CHADEMA na NCCR-M kuongoza Halmashauri ya Wilaya Uvinza. Ni
jaribio la demokrasia, Hekima na Maamuzi.
chanzo:azimio letu
0 comments: