JK AANZA KUWASHUGHULIKIA WATUHUMIWA WA ESCROW
Rais Dk. Jakaya Kikwete.
--Waziri
wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo tumemuweka kiporo, kuna
uchunguzi nimeagiza ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya
maadili pia wanafanya kwa ajili ya…
Rais Dk. Jakaya Kikwete.
--Waziri
wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo tumemuweka kiporo, kuna
uchunguzi nimeagiza ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya
maadili pia wanafanya kwa ajili ya kupata maamuzi kwa misingi ya haki.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Tibaijuka.
--Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Tibaijuka, tumekaa nae
na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa ajili gani na amesema ni za
shule, mengi yameelezwa. Maswali makubwa kwa nini hazijaenda shuleni
moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema ndo masharti ya mtoaji,
tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa kimaadili kuhusu kupokea
hizi pesa, tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue
mwingine.
--Mwanasheria
Mkuu wa serikali, Jaji Fredreck Werema ameshajiuzulu na amesema amebeba
dhamana hiyo pia kwa niaba ya waliojiuzulu.
--Kuhusu
watu kuwawajibisha, bodi ya TANESCO bahati nzuri imemaliza muda wake na
tumeanza mchakato wa bodi, na tutaipata siku chache zijazo. Katibu mkuu
wa wizara ni mtumishi wa umma, hivyo kuna taratibu na nimeshaagiza
zianze.
----Serikali
iandae muswada wa sheria ulioleta TAKUKURU, ni wazo zuri, Mchakato wa
kufanya mageuzi TAKUKURU tumeuanza tangu 2008. Sheria ya kwanza ya PCCB
ilikua na makosa manne tu ya rushwa tukayaongeza mpaka 24.
--Kuhusu
mabenki kuwekwa kama zinatakatisha fedha, pendekezo uchunguzi ufanyike
ni pendekezo zuri na intelligence unit ndio watakaofatilia
--Rais
aunde tume ya kijaji kuwachunguza majaji(Mujulizi na Luangisa),
nimelipokea lakini utaratibu wa kisheria kushughulikia linatakiwa
lianzie kwenye mahakama na sio linaanzia kwa rais au bunge. Mahakama
inaporidhika amepoteza sifa, inaletwa kwa rais maana ndie anaeteua
majaji. Lazima kushirikiana na muhumili wenyewe. Nilichosema tumwachie
jaji mkuu na wakiridhika watakuja kwa raisi endapo wataridhika wahusika
wamekosa sifa.
--Kamati za bunge kuwavua nyadhifa wenyeviti wa kamati za bunge tunaliachia bunge lenyewe
--TAKUKURU na jeshi la usalama vichukue hatua, nimeshaeleza hatua zinaendelea.
--Kuhusu
uwazi wa mikataba na mapitio, tutafanya na lipo moja tutafanya kuhusu
usiri wao wa biashara, kuweka wazi zinaweza kutumiwa na wapinzani wa
kibiashara, hivyo tutaangalia namna ya kulifanya.
--Niwahakikishie mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira katika kutimiza maazimio ya bunge.
Kutaifisha mitambo ya IPTL, tunahimiza sekta binafsi kuwekeza, tunapotaifisha habari tunayopeleka si nzuri, sisi tuliotaifisha mwanzo siku hizi tunasema hatuna sera ya ujamaa hivyo waje kuwekeza. Watasema wale jamaa wamerudia tena wanataifisha. Mahakama imefanya maamuzi kwa IPTL, kwanza waibadili mitambo yao ibadili itumie gas badala ya mafuta, tukiyafatilia yanaweza kutufikisha mahali. Haya ya kutaifisha yananipa wasiwasi
Kutaifisha mitambo ya IPTL, tunahimiza sekta binafsi kuwekeza, tunapotaifisha habari tunayopeleka si nzuri, sisi tuliotaifisha mwanzo siku hizi tunasema hatuna sera ya ujamaa hivyo waje kuwekeza. Watasema wale jamaa wamerudia tena wanataifisha. Mahakama imefanya maamuzi kwa IPTL, kwanza waibadili mitambo yao ibadili itumie gas badala ya mafuta, tukiyafatilia yanaweza kutufikisha mahali. Haya ya kutaifisha yananipa wasiwasi
--Maazimio ya bunge
Kwanza niseme serikali imayakubali na niwapongeze waheshimiwa wabunge. Nashukuru kamati ya bunge chini ya Zitto na Filikunjombe, watu wa upinzani kufanya yale maamuzi yao, kwamba CCM ni mafisadi. Ni kweli watu hawa wanatoka CCM ila sio kwamba CCM inaridhia. Ntashangaa mbunge kulipinga hili eti kisa tu yuko CCM, bunge wengi ni CCM, kama ni kweli walikuwa hawataki hakuna azimio lingepita? Na kuna baadhi ya wabunge wa CCM waliudhika na maovu haya, wenzetu wanatafuta sifa laini kwa jambo ambalo ni letu sote.
Kwanza niseme serikali imayakubali na niwapongeze waheshimiwa wabunge. Nashukuru kamati ya bunge chini ya Zitto na Filikunjombe, watu wa upinzani kufanya yale maamuzi yao, kwamba CCM ni mafisadi. Ni kweli watu hawa wanatoka CCM ila sio kwamba CCM inaridhia. Ntashangaa mbunge kulipinga hili eti kisa tu yuko CCM, bunge wengi ni CCM, kama ni kweli walikuwa hawataki hakuna azimio lingepita? Na kuna baadhi ya wabunge wa CCM waliudhika na maovu haya, wenzetu wanatafuta sifa laini kwa jambo ambalo ni letu sote.
--VIP
walipouza na kupata dola milioni 78, wamelipa kodi bilioni 38. Kulikua
na tuhuma za rushwa katika mchakato mzima. Yamesemwa mengi na bado
hatujamaliza kuyasoma, rushwa ni kosa la jinai. Nilielekeza taarifa
walizozipata wazipeleke PCCB. Nimeambiwa wanaendelea na mchakato wao.
Kwa miamala, serikali inashughulika na watumishi wa umma kwa mujibu wa
taratibu, maaskofu na masheikh kupewa kitu hawatuhusu, mtumishi wa umma
ana masharti ya kupokea fedha. Watahojiwa na PCCB. Hushtuki asubuhi
akaunti ina bilioni 1.6, milioni 80 etc. Zimeanguka kutoka juu ya mti.
Huo ndo utangulizi.
--Tulitaka
kufanya uchunguzi sisi wenyewe na mamlaka zetu na taarifa zimeshakuja,
tunazifanyia kazi. Kuna vitu vimetokea, kuna vilivyofanyika nje na
taarifa hazikuja na sasa tunalaumiana, hivyo tunafanya uchunguzi na wote
waliohusuka tunawahoji na mahakama kuu ipo kesi ya PAP kumiliki hisa za
IPTL, ipo kesi ya uhalali wa PAP kupokea pesa za IPTL. Hatutaki
kuwaingilia ila sisi tutafanya uchunguzi wetu kwa ajili ya taarifa zetu.
Tuwe na uhakika hizi hisa zimeuzwa kwa bei gani, tunataka kujiridhisha
kwa sababu ipo kodi ya serikali(capital gain) na inalipwa na alieuza na
sio alieuziwa. Kodi hulipwa na aliepata na sio aliepoteza (Alienunua).
--Fedha
zilizotoka imelipwa PAP, akitokea mtu ana madai, serikali mnaikinga
vipi. Ingetokea mtu ana madai yoyote angepelekwa PAP kulingana na
makubaliano. Kukawa kuna hoja kuwa hata PAP umiliki wake wa hisa 70%
unatia mashaka kutoka Mechmar, lakini waliziuza kwanza kwa kampuni ya
Uingereza ambayo yenyewe ndo ikaziuza PAP. Kampuni ilikua chini ya
ufilisi na kwa mujibu wa taratibu huwezi kuuza ukiwa chini ya ufilisi,
kwa mujibu wa taarifa sio kweli.
--Kwa
upande wa kodi ya serikali ambazo hazikulipwa, AG alipoulizwa alisema
hakuna kodi iliyochelewa kulipwa. Mgogoro ni baina ya IPTL na TANESCO
havyo uamuzi wa standard charted haukuweza kuingia, kwa vile
haikuhusishwa, ilienda kuzuia maamuzi hayo.
--Kabla
ya mzozo wa ukokotoaji TANESCO ilikuwa inailipa ITPL Moja kwa moja.
Lakini hata ulipotokea mzozo bado IPTL haikuacha kupeleka madai na
Tanesco haikuacha kulipa. Kuwepo kwa akaunti ya escrow haibadili mwenye
fedha yake.
--Nilipokutana
na mwanasheria mkuu, alisema hakukosea katika ushauri wake na wala
mahakama haikufanya makosa, na kuhusu ile hasara amesema hakuna hasara
yyte iliyopatikana kwa sababu pesa imelipwa kwa mtu halali.
--Jambo
moja ambalo ni bahati mbaya, ilijengeka dhana kuwa akaunti kufungwa ni
jambo lililoanzishwa na maafisa wa serikali kwa manufaa yao binafsi.
--Na
hata TANESCO alipewa ushauri huo huo, uamuzi ule umetiliwa shaka na
kuonekana haukuwa sahihi na umeitia hasara nchi. Ukaibua hisia na ni kwa
sababu nzuri tu kwamba si bure na iko namna kama ya rushwa na watu
kunufaika binafsi. Mara kuna watu wameenda benki na kubeba pesa kwenye
sandarusi, lumbesa na mengineyo.
--Mfilisi
aliagizwa kuhamisha kwa PAP kutoka IPTL ikiwemo Akaunti ya Escrow,
ilizua mjadala mkali. Wizara ya nishati ilimwandikia mwanasheria mkuu
kuomba ushauri, Mwanasheria akasema lipeni, uamuzi uko sawa na hauna
matatizo na benki kuu wakauliza maswali hayo hayo na majibu yakawa
yaleyale. Kuzingatia ushauri huo akaunti ikafungwa na pesa kukabidhiwa
PAP. Mjadala ukaendelea bunguni na kwenye mablogu.
--CAG
aliwaelekeza TANESCO kuacha kuhesabu pesa walizolipa kwenye akaunti ya
escrow kama pesa zao, pesa hazikufikia sifa kuhesabika kama mali ya
TANESCO(Asset). Mahakama kuu ya Tanzania ilifanya uamuzi katika shauri
la maombi ya VIP, kusimamisha mchakato wa ufilisi wa IPTL na mahakama
ikakubali.
--Kama
katika fedha hizo ipo kodi ya serikali, kwa mujibu kulikua na kodi ya
ongezeko la thamani ambayo haikulipwa, IPTL hawakuilipa na uthamini
ulikua bilioni 21 na ushee, TRA imepeleka madai yake kwa PAP.
--Kama
mgogoro ungetatuliwa na madai ya TANESCO yakakubali ya tozo kupunguzwa,
kiasi kilichopunguzwa kuna pesa za TANESCO ambazo lazima zirudi kwa
kiasi kilichopunguzwa. Bahati mbaya miaka saba baadae halikuwa
limefanyika.
--Kimsingi
fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, mdhibiti wa hesabu
alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL, Nilipomuuliza
maana, akasema zamani walikua wanalipa moja kwa moja lakini baada ya
mzozo walikubaliana kwanza waziweke BoT.
--Akaunti
ikafunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka tozo ya uwekezaji, zinahifadhiwa
ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao lakini kabla
ya hapo TANESCO walikua wanalipa moja kwa moja.
--Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL
Nianze kuelezea ya Escrow ni kitu gani, ni tofauti kidogo na akauti zetu tatu tulizozizoea, na akauti maalumu na kazi maalumu pia ikiisha na yenyewe inafungwa, inasimamia na wakala na wakala pia anajukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.
Nianze kuelezea ya Escrow ni kitu gani, ni tofauti kidogo na akauti zetu tatu tulizozizoea, na akauti maalumu na kazi maalumu pia ikiisha na yenyewe inafungwa, inasimamia na wakala na wakala pia anajukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.
--Kwa
mujibu wa mkataba, TANESCO isipolipa inatozwa riba ya 2%, kwa mujibu wa
taarifa akaunti ilikua na 202.9 bilioni na sio 309.7, hizi zilipaswa
kuwepo endapo TANESCO ingelipa zote kwa wakati.
--Masharti
ilikuwa kampuni ya IPTL itaendelea kupeleka madai yake TANESCO ya tozo
ya uwekezaji na TANESCO itaendelea kulipa lakini yataenda escrow akaunti
badala ya IPTL lakini ya umeme yaliendelea
kwenda IPTL na ilifunguliwa 2006 na mpaka kesi kuamuliwa 2013 wakati
IPTL inachukuliwa na PAP walikua hawajamalizana. (They decided to manage
the crisis rather than resolve it)
--TANESCO
na IPTL walikubaliana kuanzisha Akaunti ya Tegeta Escrow benki kuu na
kuingia mkataba, wizara ya madini kwa niaba ya TANESCO na IPTL na benki
kuu kama wakala.
--Rais Kikwete anaelezea kuhusu mgogoro kati ya Tanesco na IPTL mpaka kupelekea kufunguliwa kwa Akaunti ya Escrow
--Aeleza
kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa naye aliagizwa na
serikali kufuatilia mihamala ya Escrow na kuchukua hatua stahiki.
--Aaanza kuelezea uamuzi wa Serikali kumtaka CAG kufanya uchunguzi kuhusu akaunti ya Escrow na taarifa kupelekwa bungeni.
--Asema amelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa wale wote waliochangia vurugu katika uchaguzi huo.
--Aelezea
furaha yake kuhusu uamuzi wa Mhe. Wassira kuwachukulia hatua wote
waliochangia kasoro za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwemo baadhi ya
watendaji kufukuzwa kazi huku wengine wakishushwa vyeo.
--Aongelea kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
--Mhe Kikwete aanza kwa kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa zawadi ya ujenzi wa maabara pamoja na kumtakia heri kuhusu afya yake.
--Rais
Kikwete ameanza kuongea na wazee wa Mkoa wa Dar katika Ukumbi wa
Diamond Jubilee ambapo Watanzania wanataraji atoe mwongozo kuhusu sakata
la Akaunti ya Tegeta Escrow na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Chanzo:bongondiyo
0 comments: