Kibarua kinachomkabili Rais Uhuru Kenyatta
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhutubia taifa kwa mara nyingine
baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kufanya shambulizi lengine la kinyama
katika mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Shambulizi
lililolfanywa Jumanne asubuhi dhidi ya wafanyakazi wa mgodini mjini
Madera Kaskazini mwa Kenya, limetokea siku kumi baada ya shambulizi
lengine kama hilo dhidi ya basi lililokuwa limewabeba wasafriki wengi
wakiwemo walimu kutoka Mandera.Watu 28 waliuawa katika shambulizi la kwanza wiki jana.
Mji huu wa Mandera unapakana na Somalia na Ethiopia. Mandera ni mji wenye idadi kubwa ya wakenya wenye asili ya kisomali wengi ambao ni waisilamu.
Wengi wa wafnyakazi hao ni walimu na wauguzi na wachimba migodi lakini kwa sasa wameanza kuutoroka mji huo baada ya shambulizi la wiki jana.
Tetesi zinasema hali hii ya watu kutoroka na kurejea makwao huenda ikaendelea.
Punde baada ya mashambulizi ya wiki jana , mshauri wa Rais anayetoka Mandera, Abdikadir Mohamed alionya kuwa kundi la Al Shabaab linajaribu kuanzisha vita kwa msingi wa dini.
Serikali ya Kenya nayo imelaumiwa kwa kukosa kuchukua hatua za kutosha kudhibiti usalama na shambulizi la hivi karibuni bila shaka litamuongeza shinikizo Rais Kenyatta za kukabiliana na mashambulizi hayo.
Upinzani umekuwa ukitoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kujizulu hasa kwa kuwa ameshindwa kukabiliana na hali ya utovu wa usalama nchini humo. Hata hivyo Rais Kenyatta emekuwa akisisitiza kwamba kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha usalama unan
chanzo:bbcswahili

0 comments: