ASLAY ..................... Mmmmmh
SABABU ZA ASLAY KUMUWEKA HADHARANI MPENZI WAKE ZATAJWA
Aslay kupitia kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika katika ukurasa wa Facebook wa EATV kila Jumatano, amesema moja ya sababu ya kuweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi ni kutokana na usumbufu mkubwa ambao amekuwa akiupata kutoka kwa watoto wa kike. “Nimeamua kuweka mahusiano yangu ya mapenzi wazi sababu nasumbuliwa sana, nahisi kufanya hivyo wataelewa na kuacha, yaani kama nimewapunguzia speed ya usumbufu”
Huyu ndiye mrembo aliyeuteka moyo wa Aslay
Swali lingine ambalo mashabiki walimuuliza ni kuhusu tetesi walizowahi kuzisikia kuwa Wema Sepetu alikuwa akimtaka kimapenzi. Aslay alijibu kuwa tetesi hizo si za kweli na ni sababu nyingine iliyomfanya amuweke hadharani mpenzi wake ili watu wamfahamu na kuacha kuzusha.
“Watu wanakuwa wanaongea mambo mengi juu ya maisha yangu hususani katika mahusiano na kusambaza taarifa zisizo na ukweli, mfano watu wanasema natoka kimapenzi na Wema huo siyo ukweli kabisaa bali Wema ni kama dada yangu, ila kutokana na mambo haya ndipo niliamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kila mtu ajue kuwa nipo kwenye mahusiano na mtu fulani na waache kusambaza taarifa zisizo na ukweli.”
chanzo:eddy bloy
![http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif](http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif)
0 comments: