Wanakijiji watarajia Rais Obama kwa hamu.
Rais Barack Obama anatarajiwa kutembelea Kenya mwishoni mwa mwezi
Julai, kwa mara ya kwanza akiwa rais tangu kuchukua madaraka 2008.
Wakazi wa kijiji anakotoka babake cha Kogelo, magharibi mwa nchi
wanatarajia atawatembelea.
Kogelo ni kijiji kidogo alikozaliwa mzee Barack Obama. Kijiji hicho hakikuwa kikijulikana wala kuwa na huduma muhimu kama maji na umeme, kama vijiji vingine nchini humo, hadi pale Bw Obama alipochaguliwa kuwa seneta miaka 10 iliyopita. Hivi sasa kijiji hicho kina umeme, barabara ya lami na shule.
Na tangu wakati huo wazazi wa kijiji wamewaandikisha watoto wao kwenda shule kwa wingi na hata kuna shule ambayo imeundwa katika uwanja asilia wa familia ya Obama iliyopewa jina Senetor Obama Primary School.
Katika shule hiyo wanafunzi wana matumaini makubwa ya kufanikiwa, wakipewa fursa ya kusoma kulingana na mkuu wa shule Bw Manasseh Oyucho.
Katika shule hiyo pekee, mnamo muongo mmoja uliopita, idadi ya walioandikishwa imeongezeka maradufu.County ya Siaya, ambako kijiji cha Kogelo kinapatikana imetumia takriban shilingi milioni 52 kufanya matayarisho ya kumpokea mtoto wao. Na wakazi wa kijiji wanasema wanamatumaini madogo kuwa kiongozi huyo wa taifa kuu la dunia kama atapata muda kuwatembelea
chanzo:voaswahili

0 comments: