POLISI WAIKEMEA CCM BAADA YA KUZIDISHA MUDA WA KAMPENI,
Jeshi
la Polisi nchini Tanzania limesema kuwa litatoa tamko la jeshi hilo juu
ya Chama cha Mapinduzi kuzidisha muda wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za
chama hicho wiki iliyopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa mdahalo wa wadau wa uchaguzi jana
jijini Dar es salaam Kamishna wa Mafunzo na Operasheni wa Jeshi la
Polisi CP Paul Chagonja amesema kuwa wanashughulikia suala hilo na muda ukifika watatoa tamko.
Ameongeza kuwa ili uchaguzi uwe wa Amani ni lazima watu wote watimize wajibu wao.
Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwakilishwa na Jaji Mstaafu John Mkwawa
alivitaka vyama vya siasa kuzingatia maadili ya uchaguzi waliosaini ili
kulinda amani na kuepusha migogoro na uvunjifu wa Amani.
chanzo:http://modesigntz.blogspot.com
0 comments: