Soma ya Lipumba hapa ukweli upo hapa
Lipumba ajiuzulu uenyekiti wa CUF
Pigo jingine kubwa ndani ya UKAWA lilitokea Alhamis baada ya kumsimamisha Bwana Edward Lowassa kama mgombea wake wa urais na Juma Duni Haji kama mgombea mwenza, sasa mwenyekiti mwenza wa umoja huo na mwenyekiti wa taifa wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya chama hicho cha CUF.
Bwana Lipumba alitoa uamuzi huo mapema Alhamis baada ya kuzuka sintofahamu ya hatima yake ndani ya CUF katika siku kadhaa zilizopita.
Akiwa amefuatana na watu wawili ambao hawakutambulika mara moja Profesa Lipumba alifika katika hotel ya Peacock ya jijini Dar Es Salaam akiwa ameshika mkoba uliokuwa na katiba iliyopo sasa na katiba inayopendekezwa kisha alianza kutoa historia ya kujiunga kwake na harakati za kukiongoza chama hicho mpaka hivi sasa na kueleza kuwa dhamira yake ndiyo inamsuta kutokana na kile alichodai kuwa viongozi walioingizwa katika UKAWA kwa sasa ndio walewale waliokuwa wanapinga katiba Pendekezwa iliyoandaliwa na jaji Warioba.
Hata hivyo Profesa Lipumba aliwaomba radhi wanachama wake na wananchi kwa uamuzi wake huo wa ghafla katika kipindi hiki ambacho walikuwa na matumaini ya mabadiliko
Profesa Lipumba alielezea hatma yake sasa baada ya kujiuzulu wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Wakati huo huo katibu mkuu wa chama cha Maendeleo na Demokrasia-CHADEMA Wilbroad Slaa naye alitangazwa kupumzishwa ili kutafakari hatma yake baada ya madai kwamba hakuridhishwa na utaratibu wa kumpata mgombea wa urais ndani ya Umoja huo.
0 comments: