DR. SHEIN AZINDUA MNARA WA MIAKA 50 YA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR
Haiba
ya Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka Hamsini ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar ya Mwaka 1964 inavyoonekana baada ya kumalizika kujengwa hapo
katika Majumba ya Maendeleo Michenzani Mjini Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein
akikata utepe kuashirika kuufungua Rasmi Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka
50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Michenzani Mjini
Zanzibar.
Mshauri
wa Ujenzi wa Mnara wa wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar Mhandisi Abdul Aziz akimpatia maelezo Rais wa Zanzibar Dr.
Shein wakati akiukagua Mnara huo baada ya kuuzindua rasmi.
Rais
wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein akiangalia mandhari ya Mji wa
Zanzibar katika chombo maalum { Darubini } wakati alipotembelea sehemu
mbali mbali za Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Michenzani baada ya Kuuzindua rasmi.
Mandhari
ya Bustani ya Michenzani iliyomo ndani ya eneo la Mnara linavyoonekana
kwa juu ya Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein
amewatahadharisha watu wanaoogopa mabadiliko ya Maendeleo kwamba
waachane na tabia hiyo vyenginevyo Dunia bila ya shaka na ajizi
itawabadilisha.
Alisema Wazanzibari wanapaswa kwenda na wakati katika kuendesha pamoja
na kusimamia masuala yao ili waende sambamba na wananchi wa visiwa
vyengine Duniani wanaoonekana kupiga hatua za haraka za Maendelei ya
Kiuchuni na Ustawi wa Jamii.
Dr. Ali Mohammed Shein alieleza hayo wakati akizungumza na Watu wa rika
mbali mbali ambao wengi wao ni vjana na Watoto mara baada ya kuuzindua
Mnara wa Miaka 50 ya Mapinduzi Matukjufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964
uliojengwa katika Majumbe ya Maendeleo Michenzaji Kati Kati ya Mji wa
Zanzibar.
Alisema wapo watu wakiwemo baadhi ya watendaji wa Taasisi za Umma wenye
madaraka ya kutoa maamuzi ambao wana tabia ya kuogopa Mabadiliko kwa
kuchelewesha kuidhinisha miradi ya Kiuchumi inayokusudiwa kuwanzishwa na
wawekezaji walioamua kuwekeza hapa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar alikemea kwamba tabia hiyo mbaya isiyo na sababu za
kimsingi imekuwa ikichelewesha na kuviza Maendeleo ya Wananchi na
kupunguza Mapato ya Taifa kupitia uanzishwaji wa miradi hiyo wakati
Serikal tayri imeshaweka milango wazi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya
Nchi.
Aliupongeza Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar chini ya
usimamizi wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo kwa juhudi iliyochukuwa ya
kujenga mnara huo wenye urefu wa Mita 33.5 ambao utatoa fursda kwa
wananchi na wageni kuona mamdhari nzuri ya Mji wa Zanzibar sambamba na
kupata huduma za msingi.
Alisema chimbuko la Mnara huo lililoibuliwa na Baraza la Mapinduzi
Zanzibar wakati wa maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar lilikuwa na lengo la kuonyesha vugu vugu la Maendelei ya
Zanzibar tokea kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Tarehe 12 Januari
Mwaka 1964.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar {ZSSF }
Nd. Abdulwakil Haji Hafidh alisema ujenzi wa Mnara huo mbali ya kutoa
fursa kwa wananachi na wageni kuangalia mamdhari ya Mji wa Zanzibar
lakini pia utatoa nafasi kwa wazazi kupata mapumziko huku wakiwasubiri
watoto wao wanaowapeleka katika Viwanja vya Kufurahishia Watoto
Kariakoo.
Alisema tahadhari hiyo imechukuliwa maalum kwa kuzingatia kwamba Mji wa
Zanzibar bado haujawa na maeneo mengi ya kupumzikia kiasi cha kuongezwa
maeneo hayo ili kukidhi mahitaji kwa siku zinazotokea kuwa na idadi
kubwa ya watu hasa siku za siku kuu ambazo watu wengi huamua kutembelea
viwanja hivyo.
Mkurugenzi huyo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF }
alifahamisha kwamba mnara huo utakuwa na sehemu maalum zitakazowekwa kwa
ajili ya watu na wageni kujifunza Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar,
sehemu za kujifunza wachezaji wa michezo mbali mbali maarufu duniani,
kuangalia mandhari ya Mji wa Zanzibar pamoja na Mkahawa unaozunguuka.
Alisema taasisi za Fedha kama Benki ya Wananachi wa Zanzibar PBZ, na Ile
na NMB zitatoa huduma za fedha kwa kutumia mtandao wa ATM ili
kuwaondoshea usumbufu wateja wao wakati wanapoishiwa na Matumizi.
Nd. Abdulwakili alieleza kwamba katika kulibadilisha eneo hilo la
Michenzaji Mfuko huo umeshaandaa mpango wa kujenga majengo la Kimataifa
ya Kibiashara { SHOOPING MALLS } upande wa Kaskazini kwa kutafuta
washikika wa Maendeleo watakaoshirikiana katika kujenga majengo hayo.
Mnara huo wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar wenye
ghorofa 9 uliojengwa kwa gharama ya Shilingi za Kitanzania Bilioni Nane
unatarajiwa kurejesha thamani ya Fedha hizo katika kipindi cha miaka 12
ijayo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
chanzo:matukio na vijana blog
0 comments: