EDWARD LOWASSA ATAMKA HAYA JANA.
MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO
1: Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na
kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo, katika majimbo manne
kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika
kujumlisha matokeo uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi,
majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe.
———-
2: Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi,
kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha
kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya
msingi ambayo iko kwenye sheria. Kwenye baadhi ya majimbo, ikiwemo
Nyamagana, wapinzani walipewa haki ya kura kuhesabiwa upya. Kwa msingi
huo, CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika
majimbo haya.
———-
3: Tunataka sote tujiridhishe kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa,
bado tunaendelea kukusanya taarifa za maeneo mengine kama kulikuwa na
ukiukwaji mkubwa uliobadilisha matakwa ya wapiga kura, hata hivyo
tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza viti vya Ubunge,
tumepoteza kihalali, hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi
na tutafanya tathmini baada ya uchaguzi ili tubaini makosa na
kuyarekebisha.
MAONI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI
4: CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi wa uchaguzi, tumefarijika
kwamba karibu wote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huu ulikuwa
wa haki na huru uliofanyika kwa uwazi na kwa amani na kwamba changamoto
zilizojitokeza ni ndogo na zimetokea katika maeneo machache kiasi
zisingeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa sasa.
———-
5: Tumepokea mapendekezo waliyoyatoa kwa wadau mbalimbali kuhusu namna
ya kuboresha mchakato wa uchaguzi kwa miaka ijayo, na hivyo kuimarisha
demokrasia nchini mwetu. Kwa kauli za waangalizi hawa, kwamba, kwa jinsi
uchaguzi ulivyoendeshwa, matokeo yanayotangazwa sasa ni kielelezo
sahihi cha utashi wa Watanzania kuhusu viongozi wanaowataka.
———-
MALALAMIKO YA UKAWA
6: Tumesikia malalamiko ya viongozi wa UKAWA kupitia mkutano wao na
waandishi wa habari jana, tumeshangazwa na kauli kwamba hawakubali
matokeo ya Urais yanayotangazwa na Tume, hata hivyo matokeo ya Ubunge
wanayakubali na kule wanakoshinda, wanayasheherekea.
———-
7: Tunashangazwa kwasababu Tume iliyoandaa uchaguzi wa Rais ni hiyo hiyo
iliyoandaa uchaguzi wa Wabunge, wasimamizi ni walewale, vituo ni
vilevile, na sheria na taratibu zilizotumika ni zilezile, hata fomu ya
matokeo walizosaini wakala wao kwenye vituo vya kupiga kura,
zimegawanywa katika sehemu (columns) tatu: urais, ubunge na udiwani.
———–
8: Mawakala wao walisaini fomu hizo kwenye vituo vya kupiga kura.
Wameanza kuwa na matatizo na matokeo haya baada ya kuona mwelekeo wa
kushindwa. Kama mwelekeo ungekuwa tofauti, wangekuwa na imani na Tume,
wasimamizi na taratibu zote.
————
9: Tunaomba ifike pahala sasa kwamba, katika kuijenga demokrasia yetu na
kuliimarisha taifa letu, tuanze utamaduni mpya wa anayeshindwa
kunyanyua simu kumpigia anayeshinda na kumpongeza. Nafasi ya mwisho
aliyonayo mgombea wa UKAWA kuendelea kujijengea heshima katika jamii
yetu, na kuwa mwanademokrasia, ni kwa kufanya hivyo siku Dkt. Magufuli
atakapotangazwa mshindi.
————-
10: Kwetu sisi CCM, kuchagua wagombea bora na kuwanadi na kutengeneza
sera bora na kuzinadi, pamoja na rekodi yetu katika uongozi wa nchi,
ndio njia zetu pekee za ushawishi. Katika uchaguzi huu, wananchi
wamefanya maamuzi yao kwa uhuru na utashi, ikiwemo kuwaangusha mawaziri
sita ambao tuliwasimamisha kama wagombea wetu katika majimbo mbalimbali
nguvu na utashi wa wananchi umejidhihirisha katika uchaguzi huu.
————–
11: Mchakato wa uchaguzi sasa unakaribia kufikia ukingoni, tutawapata
madiwani, wabunge na Rais, tunapaswa kuendelea na maisha na tuwape
nafasi watutumikie. Jitihada tunazoziona sasa za viongozi wa UKAWA za
kuendeleza siasa za uchaguzi kwenye mitaa ya miji yetu kwa njia za
vurugu na maandamano hazikubaliki hata kidogo.
————–
12: Tunalaani kitendo cha wafuasi wa UKAWA kuchoma ofisi za CCM katika
Wilaya ya Mbozi. Amani ya nchi hii ina thamani kuliko hitaji la
madaraka la mtu yoyote. Wenzetu wa UKAWA wana haki ya kulalamika lakini
hawana haki ya kuiingiza nchi yetu machafukoni kwa kuwakusanya vijana na
kuwaingiza mitaani wafanye vurugu na kuhatarisha maisha, kuharibu mali
na kusimamisha shughuli za watu wengine. tunawaomba Watanzania waendelee
na shughuli zao kama kawaida huku kila mmoja akitambua wajibu wake wa
kuilinda amani ya nchi yetu.
MAMBO 8 YALIYOSEMWA NA EDWARD LOWASSA
1: ‘Hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu ya Rais, Wabunge na
Madiwani yanayoendelea kutangazwa nchini na tume ya taifa ya uchaguzi,
hii ni sababu upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa
matokeo haya umevurugwa kwa makusudi na Watendaji ndani ya NEC kwa
kusaidiana na wa chama cha Mapinduzi’
2: ‘Katika maeneo mengi matokeo yalikotangazwa, kilichoripotiwa kuwa
matokeo ya uchaguzi wa Rais hakifanani wala kwendana na matakwa halisi
ya Wananchi, matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na
yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM John Pombe
Magufuli’
3: ‘Katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi kura zetu zimepunguzwa na
kuongezwa kwa mgombea wa CCM… kwa aibu sana, maeneo mengine kura
zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya kura zilizopigwa, mfano
Jimbo la Mkoani na Mtambile Pemba, Makunduchi, Chambani, Kilindi na
kwengineko ni miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa sio kura za
uchaguzi mkuu wa Rais bali mzimu wa uchaguzi’
4: ‘Katika maeneo mengine likiwemo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyopo
mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi yanatofautiana na yale yaliyokusanywa
kutoka katika vituo vyote vya jimbo hilo, hali kama hii ipo kwenye
majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA, NCCR na C.U.F ama wamekua na
nguvu kubwa au wameibuka Washindi’
5: ‘Uko ushahidi wa wazi katika majimbo yote Wagombea wa UKAWA
wameshinda, tume imechelewa kutangaza matokeo ya Urais kwa sababu
zinazothibitishwa kuwepo mikakati ya hila, matukio yote haya ya NEC
kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa yamekuja baada ya jeshi la Polisi
kuvamia vituo vyetu vitatu vya kuhesabu kura na kuwakamata Wataalamu
wetu waliokua wakipokea matokeo ya nchi nzima ambako tulikua tukiongoza
kwa maeneo mbalimbali’
6: ‘Tunaamini kwa dhati kwamba uvamizi huo ulifanyika kwa makusudi kwa
malengo ya kufanikisha uchakachuaji ambao sasa tunauona ukiendelea
kufanyika kupitia matangazo yanayoendelea kutolewa na NEC, tunapenda
kuwataarifu na Jumuiya ya kimataifa kwamba hadi wakati huo uvamizi
umefanyika kura zetu za Urais zilionyesha tukiongoza kwa asilimia zaidi
ya 60 kabla hawajatunyang’anya documents zetu, computer zetu’
7: ‘Kutokana na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na
Watendaji wa NEC, mimi Edward Lowassa na mgombea mwenza, tunautangazia
Umma wa Watanzania na Jumuiya ya kimataifa kwamba hatukubaliani na
matokeo yanayotangazwa na NEC, tunataka wasitishe mara moja na kuanza
upya kuhakiki, kinachofanywa na NEC hapa ndicho kinachofanywa Zanzibar,
zinafanyika juhudi za kupora kwa hila na kwa mabavu mwelekeo wa ushindi
wa Maalim Seif’
ssource: kengete.com
0 comments: