Orodha ya matajiri marehemu Hii Hapa
Paul Walker aingia Orodha ya matajiri marehemu
Mwigizaji nyota wa
Fast & Furious Paul Walker ameingia kwenye orodha ya karibuni zaidi
ya Forbes ya wasanii marehemu wanaopata pesa nyingi zaidi.
Walker,
aliyefariki katika ajali ya barabarani 2013, alijizolea $10.5m (£6.8m)
mwaka mmoja uliopita na sasa yumo katika nambari tisa.Michael Jackson anaongoza kwa mwaka wa tatu mtawalia, akipokea $115m (£75m), ingawa ameshuka kutoka $140m alizojizolea 2014.
Elvis Presley yumo nambari ya tatu $55m (£35.8m), naye aliyetunga filamu ya Peanuts creator Charles Schulz yumo nambari nne na $40m (£26m).
Mzaliwa wa Uingereza aliye kwenye orodha hiyo ni Elizabeth Taylor katika nambari tano.
Hawa hapa ndio wasanii 13 walio kwenye orodha hiyo ya Forbes:
- Michael Jackson: $115m (£75m)
- Elvis Presley: $55m (£35.8m)
- Charles Schulz: $40m (£26m)
- Bob Marley: $21m (£13.7m)
- Elizabeth Taylor: $20m (£13m)
- Marilyn Monroe: $17m (£11m)
- John Lennon: $12m (£7.8m)
- Albert Einstein: $11m (£7.1m)
- Paul Walker: $10.5m (£6.8m)
- Bettie Page: $10m (£6.5m)
- Theodor Geisel (Dr Seuss): $9.5m (£6.1m)
- Steve McQueen: $9m (£5.8m)
- James Dean: $8.5m (£5.5m)
0 comments: