YALIYOJIRI KATIKA SHEREHE YA KUMPATA RAIS MPYA TANZANIA
HIVI NDIVYO NCHI YETU ILIVYOANDIKA HISTORIA KUBWA KUWAHI KUTOKEA KUMPATA
RAIS KUTOKA KABILA KUBWA KULIKO YOTE NA NI UJUMBE TOSHA KWA WALE
WANAOPENDA KUBADILISHA KATIBA NA KUJIONGEZEA MUDA WA KUONGOZA...HONGERA
RAISI MSTAAFU KIKWETE KWA KUONESHA UKOMAVU WA KIDEMOKRASIA
Hivi
ndivyo nchi yetu ilivyoandika historia ya kwanza kumpata rais kutoka
kabila kubwa kabisa kuliko yote, hii ni ishara wazi kabisa kuwa
watanzania hawana ukabila,Urangi wala udini Na ni watu wapenda amani
siku zote

1.12pm:Sasa rais Magufuli akiandamana na mkewe wanaondoka katika uwanja wa Uhuru baada ya kuapishwa rasmi.
1.09pm:Amewataka viongozi wa upinzani kushirikiana na serikali yake akisisitiza kuwa uchaguzi umekwisha na kwamba rais aliyechaguliwa ni John Pombe Magufuli
1.05pm:'Sasa ni kazi tu' awataka viongozi wa upinzani kushirikiana kwa lengo la kuendeleza na kuwahudumia watanzania
1.04pm:''Nashukuru wagombea wanzangu kwa kutupa chanagmoto,tumejifunza mengi kutoka kwao''.
1.03pm:''Natambua kwamba nina jukumu kubwa la kuwafanyia kazi watanzania,lakini hatahivyo tumuweke mungu mbele ili kutekeleza ahadi hizo.
1.02pm:Magufuli:Nawashkuru watanzania kwa kunichagua kwa kura nyingi ili kuongoza taifa kwa miaka mitano ijayo.
1.01apm:Magufuli:Nawashukuru viongozi mbali,mbali waliowasili hapa ili kujumuika nami katika sherehe hii muhimu.
1.00pm:Namshkuru sana mwenyezi mungu aliyetujalia kuwepo hapa pamoja na viongozi wa dini.
12.58pm:Na sasa ni wakati wa rais John Pombe Magufuli kulihutubia taifa.
11.27am:Rais Magufuli alikagua gwaride la heshima
11.23am:Mizinga 21 ya kumkaribisha rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli yapigwa
11.22am:Jeshi laomba rukhsa kutoka kwa rais mpya wa Taifa la Tanzania John Pombe Magufuli
10.55am:Makamu wa rais wa Kwanza mwanamke nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan aapishwa
10.48am:''Mimi John Pombe Magufuli naapa nitatenda kazi zangu za urais kwa mujibu wa sheria na mila na desturi za muungano wa Tanzania,ewe mwenyezi mungu nisaidie''
10.47am:Rais mteule John Pombe Magufuli aapisshwa .Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pia amewasili hapa.
10.40am:Wimbo wa Taifa la Tanzania wapigwa na baadaye bendera ya rais Kikwete itashushwa ili kuashiria mwisho wa uoingozi wake.
10.20am:Na sasa msafara wa Rais Jakaya Kikwete wawasili katika uwanja wa Uhuru .KIkwete baadaye anaonekana kuingia katika gari rasmi la gwaride katika uwanja wa uhuru na kuwapungia mkono maelfu ya wananchi waliojaa katika uwanja huo.
10.15am:Rais Mteule John Pombe Magufuli awasili katika sherehe hizo na kulakiwa na jaji mkuu Othman Chande.
9.47am:Rais wa kisiwa cha Zanzibar Dokta Ali Mohammed Shein amewasili katika uwanja wa Uhuru na anaonekana hapa akisalimiana na rais mstaafu wa Tanzania Hassan Mwinyi.Kumbuka kiongozi huyo wa Zanzibar aliongezewa mda wa kuhudumu katika kisiwa hicho baada ya tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais katika kisiwa hicho.
9.43am:Rais mteule John Pombe Magufuli atakuwa rais wa awamu ya tano kuchaguliwa nchini Tanzania tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.
9.35am:Miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa katika hafla hii ni pamoja na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye tayari ameondoka katika uwanja wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi akiandamana na Mkewe bi. Margeret Kenyatta na anatarajiwa kuwasili katika uwanja wa sherehe hizi wakati wowote kutoka sasa
9.30am:Gwaride la kijeshi tayari limejiandaa vilivyo ikiwemo wanajeshi waliovalia sare za rangi tofauti hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Wa kwanza kutuma risala za pongezi walikuwa ni:
Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi Mohammed Abdelaziz.
Katika salamu zake kwa Rais Mteule Magufuli, Bw Kagame amesema: "Kufuatia kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kukutumia Mheshimiwa salamu za dhati, pongezi na heri nyingi kwa niaba yangu mwenyewe, Serikali yangu na wananchi wa Rwanda.”
Naye Rais Abdelaziz amemwambia Rais Mteule Magufuli: “Sisi tuna uhakika kuwa chini ya uongozi wako wa busara, Tanzania itaendelea kusonga mbele na kupata maendeleo na ustawi mkubwa zaidi.”
7:10 am Viongozi wa baadhi ya mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo Jacob Zuma kutoka Afrika Kusini, Robert Mugabe kutoka Zimbabwe na Filipe Nyusi wa Msumbiji. Mhubiri mashuhuri kutoka Tanzania TB Joshua pia atahudhuria sherehe hiyo.
7:00 am Watumbuizaji wanaotarajiwa kutumbuiza wakati wa sherehe walifika uwanjani mapema na ala zao.
6:30 am Uwanja wa Uhuru umepambwa ukapambika
6:30 am Waandishi wa BBC wamo katika uwanja huo kukuletea habari kadiri zinavyochipuka.
6:30 am Sherehe ya kumuapisha Bw Magufuli inafanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais Mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli anaapishwa leo kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25.
Bw Magufuli alipata asilimia 58.46 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania

chanzo:http://mchomvunews.blogspot.com

0 comments: