MHE. BALOZI SEFUE AENDELEA KUWASISITIZA WATUMISHI WA UMMA KUVAA BEJI ZINAZOWATAMBULISHA MAJINA YAO WANAPOKUWA KATIKA MAENEO YA KAZI
Katibu
Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiwaonyesha waandishi wa
Habari (hawapo pichani) beji yenye jina lake ambayo amewaagiza watumishi
wa Umma kuivaa wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi. Balozi Sefue
alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana
na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO)
dhidi ya Standard Bank.
Na Anna Nkinda – Maelezo
Katibu
Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza
watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa
katika maeneo ya kazi.
Mhe.
Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi
wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake
ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine.
Alisema
mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea
Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza watumishi wote wa Umma kuvaa
beji zinazowatambulisha majina yao.
“Nimeamua
kuonyesha mfano kwa vitendo kufuatia agizo nililolitoa kwa watumishi wa
Umma kwa kuvaa beji inayonitambulisha jina langu , nilisema nitakuwa wa
kwanza kuvaa jina langu nimevaa. Kama mtumishi wa umma atakuwa na
mashaka ajue mimi nimeshalivaa”.
“Mtumishi
wa umma anapomuhudumia mwananchi ni lazima ajue amehudumiwa na nani,
mtumishi wa Umma akifanya kazi zake kwa kutenda haki sidhani kama
ataogopa kuvaa beji inayomtambulisha jina lake hivyo basi kama
nilivyoagiza watumishi wote wa Umma mvae beji zinazowatambulisha majina
yenu”, alisisitiza Mhe. Balozi Sefue.
Mhe.
Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar
es Salaam na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud
Office (SFO) dhidi ya Standard Bank.
chanzo: http://www.matukiotz.co.tz
0 comments: