MSD YAKARABATI JENGO LA DUKA LA DAWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KWA KASI KUBWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DK.MAGUFULI
Mafundi
wakikarabati jengo ambalo Bohari ya Dawa (MSD), itafungua duka la dawa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MSD) Dar es Salaam jana kwa
ajili ya kuhudumia wananchi kwa karibu zaidi vikiwemo vifaa tiba. Duka
hilo linatarajiwa kufunguliwa kesho kutwa.
Fundi akitoboa ukuta sehemu litakapo fungwa beseni la kunawia katika duka hilo.
Mafundi wakiendelea na ukarabati wa jengo hilo lililopo jirani na wodi ya Kibasila linalotizamana na maegesho ya magari.
Fundi akipaka rangi ndani ya jengo hilo.
Jengo la duka hilo la MSD linavyoonekana kwa nje. Hapa mafundi wakiendelea na kazi ya ukarabati.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI
ya Dawa (MSD) imejiimarisha na kuhahikisha inatekeleza kwa wakati agizo
la Rais Dk. John Magufuli la kuweka maduka ya dawa katika hospitali za
rufaa na kanda nchini.
Katika
kutekeleza agizo hilo MSD imeanza kwa kasi kubwa ya kukarabati jengo la
duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambalo
linatarajiwa kufunguliwa kesho.
Mwandishi
wa habari hii alishuhudia jana kasi kubwa ya mafundi ujenzi
wakikarabati jengo hilo ambalo awali lilikuwa likitumika kama stoo ya
kuhifadhi vitu mbalimbali vya hospitali hiyo.
Akizungumza
na vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu ufunguzi wa maduka hayo,
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laureane Bwanakunu alisema agizo la Rais la
kuitaka MSD kuanzisha duka la dawa karibu na hospitali limekuja wakati
muafaka kwani kwenye mpango mkakati wa miaka sita wa MSD tayari ilikuwa
na mpango wa kufungua maduka hayo kwa ajili ya kusogeza huduma karibu a
wananchi.
Alisema
maduka ya MSD ambayo yatafunguliwa kwenye hospitali za rufaa na kanda
yatafanya kazi masaa 24 na kuuza dawa na vifaa tiba chini ya bei ya
soko pia yatahudumia watu binafsi na wale waliopo kwenye taratibu za
Bima ya afya kote nchini.
"Ili
kudhibiti watumishi wasio waaminifu kuiba dawa MSD inafanya kazi za
uagizaji, uhifadhi na usambazaji kwa kutumia mfumo wa mtandao wa E9 na
tangu mwaka wa fedha uliopita tumeanza kuziwekea alama ya GOT bidhaa
zetu ikiwa ni pamoja na vidonge." alisema Bwanakunu.
Alisema
vidonge ambavyo tayari vimewekewa nembo ya GOT vipo 45 na wanaendelea
kuwapa maelekezo wazabuni ili vyote viwekwe alama hizo..,nembo ya
serikali inaonekana kwenye dawa za serikali kama Diclofenac, moxillin,
iprofloxacin, Contrimoxale,paracetamol,
na magnesium.
Alisema
wanatarajia kuanzisha huduma ya kutoa taarifa kwa njia ya simu pale
wananchi watakapoona kuna wizi wa dawa za serikali na kwamba wananchi
wanaelimishwa kutoa taarifa pale wanapoona dawa za serikali mitaani.
Alisema, pamoja na serikali kuanza kupunguza deni lake linalodaiwa na MSD bado inadaiwa Sh.bilioni 53.
0 comments: