SHERIA YACHUKUA NAFASI YAKE WATUHUMIWA TRA SOMA HAPA
WATUMISHI NANE WA TRA WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO
Mshitakiwa
namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, Tiagi Masamaki (katikati) na
washitakiwa wenzake wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam leo mchana baada ya kusomewa mashitaka yao.
Na Dotto Mwaibale
KASI ya utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli na Waziri
Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa imeanza kuwagusa baadhi ya watendaji wa
Serikali baada ya maofisa wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56)
kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila
ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za
kitanzania.
Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni
Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton
Mponezya (51)
Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na
Peter Vitalis ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao
wanatuhumiwa kwa makosa mawili.
Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya
kuidanganya Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni
namba 35/2015 ya uhujumu uchumi.
Ilidaiwa katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya
Juni 1 na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la
Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa sh.
bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya
Azam, baada ya kodi zote kutolewa.
Katika shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi
na Novemba 17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa
kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali
kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.
Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.
Watuhumiwa wa kesi hiyo wakiingia ndani ya gari.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi
aliwaeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa
hiyo hawatakiwi kujibu chochote kama kweli au si kweli.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi
hiyo, kwa hiyo kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika
mahakama hiyo.
"Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana," alisema Hakimu Shahidi
Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa
mahakamani hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema
anamtoto mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.
Wakili Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe
nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia
kama upelelezi utakuwa umekamilika.
Mmoja wa watuhumiwa hao akiwa ndani ya gari la Polisi.
Watuhumiwa hao waliokaa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Gari la polisi lililowabeba watuhumiwa hao likiondoka mahakamani hapo
chanzo:tanuru la fikra
0 comments: