Chris Brown Umerudia Tena.........!
Chris Brown atuhumiwa kumpiga mwanamke
Brown alikiri makosa ya kushambulia Rihanna mwaka 2009
Polisi katika jiji
la Las Vegas, Marekani wanachunguza madai kwamba mwanamuziki mashuhuri
wa R&B Chris Brown alimpiga mwanamke Jumamosi.
Mwanamke huyo anadai msanii huyo alimgonga usoni alipojaribu kumpiga picha.Kisa hicho kinadaiwa kutokea katika hoteli alimokuwa Chris Brown mapema Jumamosi asubuhi.
Mwanamuziki huyo hajazungumza lolote kuhusiana na madai hayo.
chanzo:bbcswahili
0 comments: