Akamatwa kwa kuipelelezea Korea Kusini
Raia wa Marekani
aliyekamatwa nchini Korea Kaskazini amesema kuwa aliiba siri za kijeshi
za Korea kaskazini ili kuisaidia Korea Kusini katika taarifa na
waandishi wa habari ilioandaliwa na Pyongyang.
Kim Dong Chul mwenye umri wa miaka 62 alikiri kufanya hivyo siku ya ijumaa,akiomba msamaha kwa kupeleleza.
Bwana
Kim awali aliwaambia waandishi kwamba yeye ni raia wa Marekani
aliyezaliwa nchini Korea Kusini na kwamba alikamatwa mwezi Oktoba kwa
kufanya upelelezi.
Bwana Kim amesema kwamba alikutakana na maafisa wa
upelelezi kutoka Korea Kusini mwaka 2011 ili kuifanyia
uchunguzi,kulingana na shirika la habari la KCNA kutoka nchini Korea
Kaskazini.
Alikamatwa wakati alipokuwa akichukua habari za kijasusi za kijeshi na zile za kinyuklia kutoka kwa mtu ambaye hakutajwa.
chanzo:bbcswahili
0 comments: