SUDANI KUSINI MAMBO YAANZA KUWA SAFI, SERIKALI YAUNDWA
Rais wa Sudan
Kusini Salva Kiir amelivunja bunge lake na kuunda serikali ya umoja,
katika harakati za kupiga jeki makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza
vita vya wenyewe kwa wenyewe vya takriban miaka miwili.
Mpango huo unaowashirikisha waliokuwa waasi katika serikali ulitangazwa Alhamisi katika runinga ya taifa.
Thuluthi
moja ya mawaziri wa bunge hilo jipya ni wanachama wa chama cha SPLM-IO
kilichobuniwa na aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar,ambaye alirudi
mjini Juba mapema wiki hii ili kuapishwa kuwa makamu wa kwanza wa rais.
Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aliunga mkono hatua hiyo kama ya kihistoria katika makubaliano hayo ya amani.
Makumi
ya maelfu wameuawa na watu milioni 2 wakiwachwa bila makao katika
mgogoro huo wa Sudan Kusini ambayo ilipata uhuru wake mwaka 2011.
Mwandani
wa rais Salva Kiir Kuol Manyang atasalia kuwa waziri wa Ulinzi na David
Deng Athorbei akiwa waziri wa fedha ambao watajaribu kuimarisha uchumi
ulioathiriwa na vita vya zaidi ya miaka miwili.
Wizara muhimu ya mafuta ilipewa Dak Duop Bichok.
Wizara ya kigeni imechukuliwa na Deng Alor wadhfa
alioshikilia chini ya serikali moja ya Sudan kabla ya Sudan Kusini
kupata uhuru wake mwaka 2011.
Alor alikuwa mwanachama wa kundi
linalojiita ''wafungwa wa zamani'',viongozi wenye ushawishi waliokamatwa
wakati vita vilipoanza,lakini baadaye wakaachiliwa baada ya shinikizo
kali.
Kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkubwa Lam Akol atakuwa
waziri wa kilimo na usalama wa chakula,ikiwa ni wizara muhimu ambapo
watu milioni tano wanahitaji msaada,huku maeneo mengine yakikabiliwa na
ukame.
chanzo:bbcswahili
0 comments: