TAMKO LA RAIS KWA POLISI
Rais wa wa
Tanzania Dkt John Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini pamoja na
ofisi ya mwendesha mashitaka kujirekebisha katika utenda kazi na
kujiepusha na kashfa.
Amesema taarifa zinaonesha jeshi la polisi
limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza
ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.
Akiongea
alipokuwa akifungua kikao cha kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa,
mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa Mikoa
na Vikosi, Dodoma ametoa mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha
zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa na sare za askari.
Aidha,
amezungumzia mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya polisi na
wawekezaji akisema baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji
kazi kwa jeshi hilo.
“Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi,
nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu, nataka
muelewe na muelewe ukweli direction (njia) ninayoitaka mimi.”
Dkt.
Magufuli pia amelitaka jeshi la polisi kujiepusha na kashfa ambazo
zimekuwa zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maafisa wa polisi kujihusisha na
biashara ya dawa za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa
ujambazi.
Kuhusu Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, amesema amekuwa
akisikitishwa sana na vitendo vya serikali kushindwa katika kesi nyingi
mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.
"Niwaombe mawakili
na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslahi ya nchi mbele, kwa
sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache,
nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana na pesa pesa, wana
misemo yao wanasema dili limepatikana,” amesema.
“Na saa nyingine
kesi inapopelekwa mahakamani wana-collude (wanakula njama) mawakili wa
serikali na mawakili wanaomtetea mhalifu, na wanapo-collude (wanapokula
njama pamoja) siku zote serikali inashindwa.
chanzo:bbcswahili
0 comments: