WAGONJWA NA MAITI WALAZWA CHUMBA KIMOJA, WAPI HAPO NDANI YA TZ HII.........!
Kukosekana kwa chumba cha kuhifadhi maiti katika
kituo cha Afya cha Bulungwa wilayani Ushetu Mkoa wa
Shinyanga kumesababisha wagonjwa kulala chumba kimoja na maiti, inapotokea mtu kafariki usiku.
Kaimu
Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk Peter Dalali amesema wanalazimika
kuwachanganya na maiti hadi ndugu wa marehemu wanapowachukua.
“Kiutaratibu siyo vyema kuwalaza wagonjwa na maiti sehemu moja, ila kutokana na ukosefu wa
chumba cha maiti tunalazimika kufanya hivyo, tunaiomba Serikali kutusaidia kutatua tatizo hilo
ili kuondoa hofu kwa wagonjwa,” amesema Dk Dalali.
Dk
Dalali amesema kituo hicho kwa siku hutoa huduma ya zaidi ya wagonjwa
50 na kulaza watano, idadi ambayo ni kubwa kwa mazingira ya kijijini na
inapaswa kupatiwa ufumbuzi.
Ametaja changamoto nyingine kuwa ni kituo kukosa jengo la mapokezi ya wagonjwa wa kutwa
(OPD) hali inayosababisha madaktari kutoa huduma kwa zamu kutokana na kutegemea ofisi moja.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Alfred Rukelegwa amesema changamoto hiyo ni kubwa
kwa kuwa awali kituo hicho kilikuwa zahanati.
Mbunge wa jimbo hilo, Elias Kwandikwa ameahidi Sh500,000 za ujenzi wa jengo jingine ili
kuondoa upungufu katika hospitali hiyo.
Pia,
ameahidi kutafuta wafadhili watakaosaidia kujenga chumba cha maiti
pamoja na kushirikisha wakazi wa wilaya hiyo kuchangia ujenzi huo.
“Tunapaswa
kulichukulia suala hili kwa uzito na kwamba kila mmoja aone kulaza
mgonjwa na maiti ndani ni jambo ambalo halikubaliki na linaloogopesha,”
amesema Kwandikwa.
chanzo:eddy blog
0 comments: