MFAHAMU MZEE MWENYE FAMILIA KUBWA TZ,WATOTO 70, WAJUKUU 300
Nchini Tanzania katika mkoa wa Arusha wilayani Monduli, mzee mwenye zaidi ya miaka 100 ana watoto zaidi ya 70 na wajukuu 300.
Mzee
Meshuko Ole Mapi, almaarufu Mzee Laibon, amelazimika kuwa na shule yake
na soko kwa ajili ya jamii yake hiyo na anasema bado ana azma ya
kuendelea kuoa,Na mwandishi wa BBC Esther Namuhisa alimtembelea mzee huyo Kaskazini mwa Tanzania.
Mwanamke mmoja anayeuza vitu vya watalii kama bangili na shanga, alimwelezea kwamba soko hilo linaundwa na wanafamilia wa mzee Laibon,na si la kawaida kama yalivyo masoko mengine,kwa sababu bidhaa zinazouzwa hapo,wateja wake huwa watalii wanaoshangazwa na maajabu ya mzee Laiboni kuwa na watoto 70 na wajukuu 300,licha na kuwa na wake wachache.
Katika eneo hilo mwandishi huyo aliona nyumba zaidi ya arobaini hivi,na chini ya mti mmoja akakutana na mzee Laiboni ambaye amepumzika
Mkalimani wake alisema kuwa mzee Laiboni ana wake wanane na takriban watoto sabini na sita mbali na wajukuu karibu mia tatu.
Kuhusu ni vipi angeweza kuhudumia familia yote hiyo licha ya umri wake alisema kwamba,wakati wa kiangazi yeye huuza ngombe na kununua mahindi
Mzee laiboni alisema kuwa wazo la ujenzi wa shule,lilijiri kwa sababu watoto wake walikua wanasoma shule ya mbali na kuna wakati walikua wakishindwa kwenda shule kutokana na tembo ambao pia waliwahi kuua mtu.
Baadaye mwandishi huyo alizuru shule ya mzee Laiboni ambapo alikutana na mwalimu mkuu wa shule hiyo.
chanzo:bbcswahili

0 comments: