Wapinzani wanyimwa chakula Zimbabwe
Tume ya haki za 
binadamu nchini zimbabwe imesema kuwa watu wanaounga mkono upinzani, 
walio kwenye  maeneo yenye ukame wamenyimwa misaada ya chakula na chama 
tawala  cha ZANU-PF.
Mwenyekiti wa bodi maalum Elasto Mugwadi, 
amesema kuwa kwa sasa uchunguzi umebainisha kuwa watu wanaounga mkono 
upande wa upinzani wanaambiwa waziwazi kuwa hawatopewa msaada wowote wa 
chakula na inaarifiwa kuwa watu wengi wameathirika kutokana na hali 
hiyo.Taarifa ya serikali inaonyesha kuwa nusu ya wakazi wa vijijini 
wamekumbwa na njaa,  jambo linalochochea kupingwa kwa utawala wa rais 
Mugabe.Wakati huo huo mahakama kuu nchini humo imebatilisha marufuku ya maandamano yaliyokatazwa na polisi kwenye mji mkuu wa Harare. Ambapo marufuku hiyo ilidumu kwa muda wa wiki mbili.
Wanaharakati wanne wanaopinga utawala wa rais Mugabe ndiyo waliwashilisha pingamizi mahakamani kupinga uamuzi wa polisi kupiga marufuku maandamano kwenye mji mkuu wa Harare.
Hakimu wa mahakama kuu ya nchini humo amesema kuwa marufuku hiyo ya polisi ilikuwa batili. Siku za hivi karibuni kumekuewa na ongezeko la wimbi la maandamano nchini Zimbabwe, wakiandamana kuhusu mdororo wa uchumi nchini humo.
Maandamano makubwa yanaratibiwa na wanaharakati kupitia mitandao ya kijamii.
chanzo:http://www.bbc.com
 
 
 
 
 
 
 
0 comments: