DC Hapi aamuru kuchunguzwa mfanyabiashara anayedaiwa kusema ‘serikali iko mfukoni mwake’
Mkuu
wa wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapileo asubuhi amewatembelea
wananchi wa Tegeta kwa ndevu eneo ambalo baadhi ya wananchi walionekana
kwenye vyombo vya habari wakilalamika kuhusu kufanyiwa hila na
mfanyabiashara mmoja ajulikanae kwa jina la Emily Reshea aliyechimba
shimo mbele ya nyumba za watu na kuziba njia za wananchi kupita kama
mbinu ya kuwalazimisha wamuuzie maeneo yao.
Hapi akiwa
katika eneo hilo akiambatana na wataalamu wa mipango miji, mhandisi wa
manispaa na askari wa jeshi la polisi ameagiza kuvunjwa kwa ukuta
ulioziba njia za wananchi kupita, kufukiwa kwa shimo lililochimbwa kabla
ya saa 12 jioni leo october 10 2016 na kumtaka OCD Kawe kuchunguza
tuhuma za mfanyabiashara huyo kudaiwa kusema kuwa “serikali iko mfukoni
mwake” na ikibainika kuwa ni kweli akamatwe mara moja na kuhojiwa na
vyombo vya dola.
chanzo: http://millardayo.com
0 comments: