" ANAYEDAI KUOMBWA RUSHWA YA NGONO AJITOKEZE HADHARANI."...HASHIM LUNDENGA
Mkurugenzi
Hashim Lundenga amesema “kuna kushutumiwa kwamba tunachukua rushwa ya
ngono kutoka kwa Wasichana kitu ambacho sio kweli, hakuna msichana
aliesema ameingia kambini au ameshinda kwa sababu ametoa rushwa ya
ngono, katiba yetu inakataza kabisa yeyote kujihusisha na hilo”
Toka Miss Tanzania ianze 1994 mpaka sasa kuna kesi zisizozidi nne za
wazazi waliokuja kuwaondoa watoto wao kwenye kushiriki mashindano hayo
baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu hizo kashfa za ngono.
Moja
ya kesi hizo ni pamoja na ya Mchungaji aliemuondoa mwanae baada ya
kupewa ubalozi wa kinywaji chenye kilevi, mrembo mwingine alikua Nadya
aliekua masomoni Chuo kikuu familia yake ilikataa kabisa mtoto wao
kushiriki.
Lundenga amesema kuna wazazi wengine ambao walieleweshwa na wakaelewa
akiwemo Mzee Muhere ambae aliposikia mtoto wake ameshinda Miss
Kinondoni aliwapigia kelele sana lakini akaeleweshwa akaelewa na sasa
mtoto wake anamiliki kampuni kubwa na anaendesha maisha vizuri kuliko
baba yake alivyodhani.
Kwa
kumalizia, Lundenga amekiri kwamba wanao utaratibu, sheria na kanuni
kwenye katiba yao ambayo imepitishwa na Serikali ikiwa na maagizo
mablimbali ikiwemo marufuku ya kiongozi yeyote kuomba rushwa ya ngono.
Pamoja
na kuzushiwa hizo kashfa, amesema idadi ya Warembo wanaotaka kushiriki
haijapungua bali imeongezeka kwa sababu Wasichana ndio wanazidi
kujitokeza.
chanzo : gumzo la jiji
0 comments: