Ethiopia kujenga bwawa kwenye Blue Nile

...................
Mto Nile

Ethiopia imeanza kuelekeza kwingine mkondo wa maji ya mto Blue Nile ili kujenga bwawa kubwa, hatua ambayo imezua mzozo mkubwa na nchi zinazotegemea maji ya mto huo.
Bwawa hilo litakalogharimu Ethiopia dola bilioni 4.7 ni sehemu ya mradi unaolenga kuigeuza Ethiopia kuwa muuzaji mkuu wa nishati ya umeme inayotengenezwa kutokana na maji.
Misri na Sudan zinasema mradi huo unakiuka makubaliano ya miongo kadhaa kuhusu matumizi ya pamoja ya maji ya mto Nile.
Mradi huo umesababisha mgogoro kati ya Ethiopia na nchi zinazotumia maji ya mto Nile.
Bwana hilo lijulikanalo kama Great Ethiopian Renaissance, ambalo tayari limeanza kujengwa ni sehemu ya mradi wa uekezaji wa dola bilioni 12 ili kuimarisha ununuzi wa kawi ya nchi hiyo.
Mto wa Blue Nile ni moja ya vyanzo vya maji ya mto Nile, moja ya mito mirefu zaidi duniani.
Misri na Sudan zinapinga ujenzi wa bwawa hilo.
Wanasema Bwawa hilo linakiuka mkataba wa enzi za kikoloni ambao unawapa 90% umiliki wa maji ya mto huo.
Bwawa la The Grand Renaissance , ambalo linajengwa katika eneo la Benishangul-Gumuz linalopakana na Sudan, hatimaye litaweza kuzalisha megawati 6,000 za umeme
kulingana na serikali ya Ethiopia.
Kiwango hiki ni karibu mara ya sita ya umeme unaozalishwa na mitambo sita ya nuklia.

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: