HATIMAYE LWAKATARE AKWAMA TENA KUPATA DHAMANA, KESI YA JAYDEE YARUSHWA MPAKA JUNE 13.

...................


Picture

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare na mwenziye Ludovick Joseph wamekwama tena leo Jumatatu, Mei 27 kupata dhamana baada ya Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu, Sundi Fimbo kueleza kuwa Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Aloyce Katemana, bado yupo likizo tangu wiki tatu zilizopita.
Watuhumiwa wanakabiliwa na shitaka la kupanga njama za kumnywesha sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.


Lady Jay Dee akiwa na mumewe Gardner Habash wakisuburi kesi kutajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kindondoni leo asubuhi saa tatu. (picha: Imma-Matukio blog)

Mwanamuziki Judith Wambura-Habash --Lady Jay Dee-- alifika katika mahakama ya Kinondoni leo kama ilivyotakiwa kwa mashitaka aliyofunguliwa hapo. Baadaye amefahamisha kuwa ameambiwa ardui tarehe 13 Juni 2013.
Kesi imetajwa tena tar 13 June 2013. Saa 5 asub.

http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: