Hotuba ya Rais Kikwete ilivyotoa picha halisi

...................



Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete
























Dar es Salaam,Tanzania
NDUGU Wadau wa tovuti  inayopendwa na wasomaji wengi ndani na nje ya nchi ya habarimpya.com ni imani yangu kwamba hamjambo na mnaendelea vyema na ujenzi wa mataifa yenu popote mlipo duniani, habarimpya.com imeamua kuwaletea hotuba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Habarimpya.com imeamuwa kuwaletea mfululilzo wa hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa mwezi April mwaka huu ili kuwakumbusha wale waliowai kuisoma na kuwajulisha wale ambao hawakuwai kuisoma.
Habarimpya.com inaamini kwamba, hotuba hiyo ya Rais Kikwete ilitoa picha halisi ya mambo mbalimbali yanayo endelea kutokea nchini Tanzania hivi sasa,katika hotuba hiyo Rais Kikwete alizungumza mambo mazito ambayo kila mtanzania anapaswa kuyazingatia na kuyatekeleza kwa mslahi na ustawi wa Taifa lao.
Ungana na Rais Kikwete katika Hotuba yake "Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kunipa fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila mwisho wa mwezi. Leo ninayo mambo matatu ninayopenda kuzungumza nanyi.
Ziara ya Rais wa China Nchini Tanzania Ndugu wananchi;
Jambo la kwanza ni ziara ya Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China aliyoifanya nchini kwetu kati ya tarehe 24 na 25 Machi, 2013. Lengo la ziara yake ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya China na Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa kumpokea vizuri mgeni wetu na ujumbe wake. Wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake.
Kwa niaba yenu, nimepokea salamu za shukrani kutoka kwa Rais Xi Jinping akielezea kufurahishwa na mapokezi mazuri tuliyowapatia. Naomba tuendelee kuonesha moyo wa upendo na ukarimu kwa wageni wetu wengine mashuhuri watakaotutembelea siku za usoni. Ndugu wananchi; Nami pia, nimemshukuru sana Mheshimiwa Xi Jinping kwa kukubali mwaliko wangu na kufanya ziara ya kihistoria na yenye mafanikio makubwa kwa nchi yetu. Ameifanyia nchi yetu jambo la heshima kubwa na kumbukumbu isiyosahaulika. Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kuitembelea, tena siku kumi tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi yake. Na, kubwa zaidi ni kutumia fursa ya ziara yake hapa nchini kutangazia dunia Sera ya China kwa Afrika katika kipindi cha uongozi wake.
Tumefarijika sana kusikia kuwa uhusiano na Afrika bado unapewa kipaumbele cha juu na viongozi wapya wa China. Pia, kuwa China itaendelea kukuza biashara na uwekezaji na kuongeza misaada ya maendeleo kwa Afrika ikiwemo kutoa nafasi 18,000 za mafunzo kwa vijana wa Kiafrika. Kama mtakumbuka nchi zetu mbili zilitiliana saini mikataka 16 ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Misaada ya maendekeo kwa maeneo yetu ya kipaumbele nayo imejumuishwa.
Ndugu Wananchi;


source;  uwanja wa fikra
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: