MADIWANI MKOANI DODOMA WAMEWASIMAMISHA KAZI BAADHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO
Wafanya Biashara za masokoni wakikusanya vitu vyao kwa
hofu ili kukimbia baada ya kushtuliwa kuwa asikari wa manispaa
wanaokamata watu wanaovunja sheria ndogondogo za manispaa wanakuja
kuwakamata katika eneo hilo la stand ya muda ya Daladala ya Oil Com
ambapo wamekuwa kero kutokana na msongamano mkubwa wanaousababisha.
..............................................................
Na John Banda,Dodoma.
MADIWANI mkoa wa
Dodoma wamewasimamisha kazi baadhi ya watumishi katika Halmashauri hiyo
kwa kushindwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuiletea hasara
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
Hali
hiyo ilijitokeza jana mkoani hapa katika kikao cha dharula cha Baraza
hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ambacho kililenga kujadili
mapendekezo ya kamati za madiwani katika vyama kuhusu hoja za ukaguzi
maalumu .
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Meya wa Manispaa ya Dodoma
Emmanuel Mwiliko alieleza kuwa baraza limeamua kupitisha kusimamishwa
kazi kwa watumishi hao wakiwemo watumishi katika tume ya Uchunguzi wa
mchakato wa zabuni ya ushuru wa soko la Saba saba.
Mwiliko
aliwataja watumishi hao kuwa ni Mkama Musese ambaye ni Mhasibu wa
mapato,Barbanas Ngungo ni mtunza vitabu vya kukusanya mapato,Paulendo
Mwasi ambaye ni Kaimu Ofisa Manunuzi na Elias Kamala Ofisa Biashara.
Aliongeza
kuwa Watumishi wengine waliosimamishwa ni waliohusika na Uendelezaji wa
viwanja vinne vya Halmashauri na Ununuzi wa gari la Halmashauri ambapo
Baraza la madiwani halikuridhika na majibu yaliyotolewa na kamati hiyo.
“Kuhusu
uendelezaji wa viwanja hivyo vinne imebainika kwamba kuna udanganyifu
katika malipo ya fedha ambazo zimekwisha lipwa kwa Mhandisi wa
Uendelezaji wa viwanja hivyo kwani katika kikao cha baraza la madiwani
majibu yaliyotolewa na Menejimenti yalionesha Mhandisi Mshauri
alishalipwa Milioni 49,257,565 wakati usahihi wa ufuatiliaji unaonesha
kuwa Mhandisi huyo allilipwa Shilingi 142,898,943.02.
“Kuhusu ununuzi wa
gari la Halmashauri iligundulika kuwa Bodi ya zabuni iliidhinisha na
kuweka mkataba wa ununuzi huo kwa shilingi 94,130,400.00 badala yake
gari hilo lilinunuliwa kwa Shilingi 154,565,250.00 na ongezeko la bei
halikupata kibali au idhini ya Bodi ya zabuni wala kikao cha kamati ya
fedha na Uongozi”alisema Mwiliko.
Aidha aliwataja
wahusika hao kuwa ni Issack Kissa Mchumi wa Manispaa,Richard Chacha Mkuu
wa Idara,Ardhi na Mipango Miji,Mukama Musese Mhasibu Daraja la
kwanza,Neema Chamgeni Mchumi Daraja la pili na Happiness Matonya Mchumi
Daraja la pili.
Hata hivyo Mwiliko
alieleza kuwa Baraza pia limependekeza iundwe tume ya Madiwani
ikijumuisha vyombo vya dola na wataalamu wa Manispaa ili mkufanya
uchunguzi wa masuala hayo pamoja na kupendekezwa kuwa wataalamu watoke
TAKUKURU,polisi,Mkaguzi wa nje na Mhandisi wa Ujenzi na sheria.
Chanzo:Demasho
0 comments: