SIASA SI MCHEZO:MKUTANO WA CCM TABORA,CHADEMA WACHEZEA KICHAPO,KEJELI NA ZOMEAZOMEA VYATAWALA!!
Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bw.Idd Ame akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara ambapo katibu huyo alikuwa akinadi Sera za CCM. |
Mmoja kati ya makada wa CCM wilaya ya Tabora mjini alikuwa akisikiliza kwa makini hotuba za baadhi ya viongozi wa CCM katika mkutano huo wa hadhara. |
Mjumbe wa NEC Bw.John Mchele naye alipata fursa ya kuzungumza na wananchi ambapo aliwataka kutokihama CCM kutokana na baadhi ya kauli za wanasiasa wanao kikejeli na kukichafua chama hicho. |
Askari
Polisi Tabora akiwaangalia kwa hasira baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa
ni Green Guard ambao walikuwa wakimsurubu kijana huyo anayedaiwa kuwa ni
wa Chadema katika vurugu zilizojitokeza baada ya zomeazomea wakati wa
mkutano wa CCM Tabora mjini.
Na (mwandishi wetu).
VIONGOZI WA CCM TABORA WAZOMEWA MKUTANONI.
CHAMA mapinduzi (CCM),na baadhi ya viongozi wake,kwa mara ya kwanza
jana walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kukumbwa na
“zomeazomea”toka kwa wanannchi kwenye mkutano wa hadhara.
Tukio la kuzomewa kwa viongozi wa wilaya na mkoa lilijiri kwenye
mkutano wa hadhara ambao ulifanyika kwenye viwanja vya stendi ya
mabasi zamani ambapo CCM ilikuwa ikifanya mkutano wake.
Mkutano huo wa hadhara unafanyika baada ya CHADEMA ikiongozwa na naibu
katibu mkuu wake,Zitto Kabwe, kufanya mkutano eneo hilo na kutamka
wabunge wa CCM Tabora hawawatendei haki wapigakura wao na CHADEMA
watapiga kambi Tabora kuwatetea wananchi kwenye haki zao.
Hatua hiyo iliwafanya CCM nao kuja na badhi ya viongozi akiwemo mbunge
wa jimbo la Tabora mjini Aden Rage kujibu mapigo.
Dalili za zomeazomea zilianza mapema kwani baadhi ya wananchi walianza
vicheko na kejeli kwa viongozi wa CCM huku wengine wakisikika na
kutamka hawataki majigambo,matusi bali wanataka barabara za lami
Tabora-Nzega,Tabora-Urambo na ile ya Itigi-Tabora na wengine 'Peoples
Power'.
Wakati katibu wa CCM mkoa wa Tabora Idd Ame,akimwaga sera
zake,wananchi wachache waliokusanyika kwenye mkutano huo walianza
kuzomea kila katibu huyo alipokuwa akikikejeli chama demokrasia na
maendeleo,(CHADEMA).
“Ndugu zangu wananchi hebu angalieni mnavyodanganywa hivi hawa CHADEMA
wanajigamba kujenga barabara wakati wao siyo watoaji wa fedha na
kwamba fedha zinatolewa na serikali ya CCM siyo hao CHADEMA wanafiki
waongo.”alisema Ame.
Wakati katibu huyo akiendelea ma sera zake huku akikejeli na kufikia
kutamka mtu anakuja anaacha jimbo lake Kigoma kuja Tabora kuwafundisha
siasa huu ni ‘upumbavu’ kabisa.
Baada ya katibu huyo kutamka maneno hayo ndipo wananchi walipoanza
kuzomea kwa nguvu na kudai wanantaka sera za siyo matuzi huku wengine
wakisema nyie CCM waongo siku zote mlikuwa wapi kuja kufanya mikutano
hadi CHADEMA waje.
Aidha zomea zomea ilizidi ambapo katibu wa CCM mkoa wa
Tabora,alipoendelea kutamka kuwa endeleeni na huo ujinga wenu hapa
tutaumizana hapa hali ambayo ilizidisha hasira za wananchi huku nao
wakijibu mapigo kuwa sawa tu tuumizane tumechoka na ahadi zenu za
uongo.
“Hapa tuko kamili endeleeni kuzomea tu……..tutaumizana kwelikweli hapa
msifikiri hatuwezi na tutawashitaki viongozi wa CHADEMA Tabora kwa
kutufanyia fujo kwenye mkutano wetu.”
Wakati katibu huyo akitamka hayo,mjumbe wa NEC John Mchele alitoka
jukwaani na kwenda kumnong`oneza katibu huyo aachane na hayo amwage
sera tu.
Baada ya hapo ndipo ilizuka fujo kubwa huku Green Gurd wa CCM
wakitembeza mkong`oto kwa baadhi ya wananchi ambao walikuwa
wakionyesha ishara ya vema ikiwa ni alama ya CHADEMA na tafrani hiyo
ilidumu kwa dakika 20 hivi na ndipo askari polisi walipoongezwa na
mkutano kuendelea.
Baada ya vurugu kutulia huku wananchi wengine wakiondoka, mbunge
Tabora mjini Aden Rage alipopanda jukwaani ni kuongea na
wananchi,ambapo alitoa sh milioni 68 kwa kata kumi za manispaa hiyo,na
kila kata ilikabidhiwa hundi yake kwa ajili ya miradi ikiwemo ujenzi
wa vyoo,umaliziaji nyumba za walimu na madarasa.
Aidha mbunge huyo alikabidhi chama wanedesha bodaboda pikipiki mbili
na kutoa ahadi ya kuendelea kuchangia misaada.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa CCM tabora mjini Moshi Abdurahaman
Nkonkota alilaani jeshi la polisi kuwa hawataki kulinda mikutano ya
CCM hadi wanafanyiwa vurugu.
Tutalipeleka lalamiko hili ngazi za juu kuwa askari polisi huwa
hawafiki kwenye mikutano ya CCM.” Alisema

chanzo : Kapipihabari.com
0 comments: