Syria yaonya Israel kutoishambulia
Rais wa Syria Bashar al-Assad ameonya Israel dhidi ya kuishambulia nchi yake katika siku za usoni.
Bwana Assad aliambia televisheni ya kitaifa ya
Syria kuwa wameafikiana na Urusi iweze kuisambazia silaha na tayari
mpango huo unatekelezwa, ingawa hakuthibitisha ikiwa tayari wameanza
kupokea silaha.Hezbollah
Wakati huohuo, mapigano makali yanaendelea katika mji muhimu wa Qusair.
Daktari mmoja ametaja tisho analokabiliwa nalo katika kuishi katika eneo hilo, akiambia BBC kuwa zaidi ya watu 600 wamejeruhiwa na wamekwama katika maeneo wanakopigania waasi na wanajeshi wa serikali.
"wanalazimika kusubiri hadi siku nne kuweza kupata maji ya kunywa na wala sio maji kwa ajili ya matumizi mengine ya kila siku kama kuosha nguo na kadhalika.''
Kuna wanawake na watoto wanaokufa katika vita hivi vya udhibiti, wa mji huu ambao uko umbali wa kilomita 30 kusini mwa mji wa Homs.
Aidha ameelezea kuona miili mingi ya wapiganaji wa Hezbollah ambalo ni vuguvugu la kisiasa nchi Lebanon.
Gen Selim Idriss, mkuu wa kikosi cha jeshi la upinzani nchini Syria,Free Syrian Army, aliambia BBC Jumatano kuwa zaidi ya wapiganaji elfu saba wa Hezbollah, wanahusika na vita vya kutaka kukomboa mji wa Qusair.
Wakati huohuo, maafisa wa Marekani na Uingereza wanachunguza madai kuwa wanawake wawili mmoja raia wa Marekani na mwingine Muingereza wameuawa nchini Syria.
Hii inafuatia ripoti iliyopeperushwa kwenye televisheni ya Syria kuhusu stakabadhi za wafanyakazi wa kigeni waliouawa wakati mapigano yalikuwa yakiendelea katika mkoa wa Idlib
Na bbcswahili
0 comments: