TAARIFA KWAVYOMBO VYA HABARI
SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA LATOA TAMKO JUU YA NGWEA NA M to The P
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba
Marehemu
alitambulika sana katika tasnia ya muziki kupitia wimbo wa GETO LANGU
TU na baadae alirekodi nyimbo nyingi zilizopendwa na jamii ya
watanzania.
Tunawaomba
watanzania wazidi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu,
Shirikisho lenu lipo imara na tunashiriki kikamilifu katika msiba huu
tukishirikiana na wadau mbali mbali.
Tunapenda
kuwatangazia kuwa Shughuli nzima ya mazishi ya mpendwa wetu ALBERT
MANGWEA zitasimamiwa na Familia ya Marehemu, Shirikisho la Muziki
kupitia chama cha Muziki wa kizazi kipya na wadau mbali mbali.
Kwa
sasa tunakamilisha taratibu zote za awali, maandalizi na ratiba mzima
itatoka baadae. Tulifanya kikao na kaka wa marehemu (KENNETH MANGWEA)
na kukubaliana kuwa msiba utakuwa MBEZI BEACH eneo la GOIG kwa sasa
tunashirikiana vyema katika kukamilisha haya.
Kama
mambo yatakwenda sawa, ikiwa ni pamoja na kuuleta mwili wa marehemu
tunatarajia kuaga siku ya Jumamosi na baadae kusafirisha kwa shughuli ya
Mazishi huko Morogoro eneo la Kihonda nyumbani kwa mama yake mzazi MAMA
DENISIA MANGWEA.
Tunaomba tushirikiane sote kwa PAMOJA katika katika kipindi hiki kigumu.
Taarifa zaidi tutawapatia baadae kadri itakavyo bidi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe.
Vile
vile tunampa pole mwanamuziki Mgaza Pembe (M TO THE P) na kuomba maombi
ya watanzania kumuombea mwanamuziki huyo ambaye aliyekuwa Afrika
Kusini na Marehemu. M TO THE P amelazwa Afrika Kusini. Tunamuombea apone
haraka.
0 comments: