Utafiti wa jeli ya kupambana na HIV
"Kuna densi kati ya virusi na
kinga ya mwili'' anasema Daktari Angela obasi kutoka taasisi ya utafiti
wa matibabu nchini Uingereza.
"Wakati tunapopata uelewa zaidi kuhusu virusi hivi ndipo tunaelewa densi hii""Kila wakati unapokuja na mbinu ya kukabliana na virusi, virusi hivi navyo vinabuni njia yake ya kupamba na Makati ule, " anaelezea mtafiti mkuu katika taasisi hiyo na ambaye amekuwa akitafiti kuhusu HIV tangu mwaka 1996.
Utafiti wa hivi karibuni kuhusu mbinu za kukabiliana na HIV, ni mafuta au jeli, ambayo inaziba sehemu muhimu ya kinga mwilini na kuzuia virusi kuingia katika seli za mwili.
Haya mafuta, yaliyozinduliwa na kikundi cha watafiti wa kimataifa kina umiuhimu mkubwa katika kuziba kuta za kinga ya mwili ambazo virusi vya HIV hupenya ili kuvamia celi za kinga ya mwilini.
""Wanawake wengi wanashindwa kujilinda dhidi ya virusi vya HIV''"
Mtafiti mkuu katika kutengezwa kwa jeli hii, ametaja matokeo ya utafiti wao kama yanayotoa matumaini makubwa.
Hata hivyo jeli hii imeweza kutumiwa tu kwa wanyama kuona ikiwa inafanya kazi itachukua muda wa miaka mitano kabla ya kutumiwa kwa binadamu.
Utafiti mwingine ambao ulifanywa awali na ambao ulitumia jeli kama huu au Microbicides, umekuwa na changamoto nyingi sana katika vita dhidi ya virusi vya HIV.Uchunguzi huu ulioleta matumaini makubwa, ya jeli za Microbicide, ulifanyika mapema miaka ya tisini, wakati jeli ijulikanayo kama (nonoxynol-9), ambayo inatumika katika mipira mingi ya condom, iliyojulikana kuua virusi vya HIV.
Lakini baada ya utafiti zaidi kufanywa, iligunduliwa kuwa , jeli hiyo ilikuwa na athari zaidi katika kuchochea maambukizi kuliko kukinga dhidi ya virisi vya HIV.
Katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, ambako janga hili limekita mizizi na ambako hali ni mbaya mno, zaidi ya asilimia 60 ya maambukizi mapya ni ya wanawake.
Daktari Obasi anasema kuwa " katika sehemu nyingi duniani, hasa katika nchi ambazo, zina visa vya maambukizi ya HIV, kuna changamoto ya usawa wa kijinsia, hali inayoifanya vigumu kwa wanawake kudhibiti vyanzo vya maambukizi."
Kwa hivyo, nyenzo za maambukizi ambazo zinadhibitiwa na wanawake, zinaweza kuwapa nguvu kulinda miili yao dhidi ya maambukizi.
Wanawake katika nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, wanakumwba na unyanyapaa wakisisitiza kutotumia Condom kwa sababu inahusishwa na ukahaba.
Kumekuwa na ripoti nyingi za polisi kuwapokonya mipira yao ya condom wanawake makahaba katika baadhi ya nchi zikiwemo Kenya, Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe ili kuzitumia kama ushahidi dhidi yao.
Mwaka 2011, jarida la New York Times, liliripoti,kuwa polisi nchini Marekani walikuwa wanatishia kuwakamata makahaba ikiwa watapatikana wanabeba zaidi ya condom mbili.
Kutafuta tiba
Tiba ya ukimwi bado , na ikiwa itapatikana basi itakuwa tu katika chanjo.Elimu kuhusu ngono na utumiaji wa mipira ya Condom ingali bado ni muhimu katika kukinga maambukizi.
16,000 nchini Thailand, na kupatikana kupunguza viwango vya maambukizi kwa thuluthi moja.
Mtafiti mkuu na mwanasayansi ambaye pia ni mshauri wa shirika la UNAIDS alisema jaribio hilo lilikuwa la kufana sana.
"Nadhani maoni yangu ni kuwa bado tuko mbali katika kupata chanjo, bado tunasubiri kupata mafanikio makubwa'' aliambia BBC
"kwa sasa watu watahitaji kuchanganya mbinu nyingi tu za utafiti ili kupata chanjo kamili siku moja''
"na hiyo haimaanishi kuwa tuwache kujilinda kama inavyosisitizwa kwa kutumia Condom na kufanya ngono salama.''
Kwa sasa hakuna tiba, lakini watafitio kama daktari Obasi wana matyumani kuwa tiba itakapatikana katika maisha yao ya utafiti. Lakini kwa sasa jeli hii ambayo mtu anajipaka mwenyewe kabla ya kitendo cha ngono, ndio silaha ya leo dhidi ya maambukizi ya HIV.
chanzo:bbcswahili
0 comments: