Taharuki mpakani mwa Israel na Lebanon
Wanajeshi wa Israel wanafanya
msako katika mpaka wake wa Kaskazini kufuatia ripoti za mashambulizi ya
roketi zinazorushwa kutoka Kusini mwa Lebanon
Shirika la habari la Lebanon limesema kuwa
makombora ya roketi yamerushwa nchini Israeli kutoka kusini mwa Lebanon.
Haijafahamika wazi ni nani aliyefyatua makombora hayo na ni wapi
yaliangukia . Jeshi la Israel linasema linachunguza taarifa hizo .Televisheni ya kundi la Hezbollah ya al-Manar imesema roketi ilirushwa ndani ya Israil usiku wa kuamia leo na kulenga mji wa kusini wa Israil unaojulikana kama Metulla.
Wakaazi wa mji huo wanasema walisikia mlipuko lakini hakuna ripoti kuhusu watu kujeruhiwa au kuuawa.
Televisheni hiyo inasema kikosi cha ulinzi cha Israil kilipelekwa katika eneo la mpakani na hadi sasa hakujatokea mashambulio yoyote. Bado haijulikani ni nani alirusha roketi hiyo.
Wachambuzi wa maswala ya usalama wanasema kuna uwezekano kuwa kundi la Hezbollah halikuhusika na huenda waliotekeleza shambulio hilo walitaka kuchochea mzozo kati ya Israil na kundi hilo.
chanzo : bbcswahili
0 comments: