MASHINDANO ya wanafunzi wa shule za sekondari(UMISETA)
mkoani Mbeya yamefunguliwa kwa simanzi kubwa baada ya mmoja wa waratibu wa
mashindano hayo kupoteza maisha katika ajali. Aliyepoteza maisha usiku wa
kuamkia leo ikiwa ni siku moja baada ya kuanza kwa mashindano hayo ni mwalimu
Abdalah Chalo(41) wa shule ya sekondari Iyunga ya jijini hapa aliyegongwa na
lori wakati akiendesha pikipiki alipokuwa akirudi nyumbani kwake muda mfupi
baada ya kukamilisha zoezi la kugawa chakula kwa washiriki wa michezo.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman mwalimu Chalo aliyekuwa
akiendesha pikipiki yenye namba T 815 BKQ aina ya King Fan alikutwa na mauti
baada ya kugongwa na lori lenye namba T 441 BYW aina ya Scania likiwa na tela
lenye namba T 496 BWD. Kamanda Athuman amesema tukio hilo lilitokea Mei 22
majira ya saa 3:00 ya usiku katika eneo la Iyunga darajani jirani na nyumbani
kwa marehemu na kumtaja dereva wa lori kuwa ni Heri Faustin(35) mkazi wa eneo
la Mama John jijini Mbeya.
Akifungua mashindano ya Umiseta alhamisi hii katika
viwanja vya shule ya sekondari Iyunga,afisa elimu mkoa wa Mbeya Juma Kaponda
amemtaja marehemu kuwa mtu aliyekuwa na mchango mkubwa katika ufundishaji wa
somo la hisabati shuleni hapo na pia usimamizi wa shughuli za michezo.
Naye
afisa michezo mkoani hapa George Mbijima amesema wamepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa za kifo cha mwalimu Chalo kwakuwa kilitokea ikiwa ni muda mfupi
umepita tangu walipokuwa katika kikao cha pamoja kabla hajawaacha na kwenda
kushughulikia shughuli ya ugawaji chakula kwa washiriki wa mashindano na kisha
kuanza safari kurudi nyumbani kwake.
Mashindano ya Umiseta kwa mkoa wa Mbeya
mwaka huu yanashirikisha jumla ya wanafunzi 1 kutoka halmashauri 1066 za mkoani
hapa lengo likiwa ni kupata wanafunzi 125 watakaounda timu ya mkoa kwaajili ya
kushiriki mashindano hayo katika ngazi ya kanda.
SOURCE:MBEYA YETU
|
0 comments: