Urusi yatetea mauzo ya silaha kwa Syria

................... Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Ryabkov amewaambia waandishi wa habari, kwamba mfumo wa makombora aina ya C-300 ambao nchi yake inaiuzia serikali ya Syria yanaweza kuzizuia nchi za magharibi kuingilia katika mzozo wa vita nchini Syria.
 Akizungumza mjini Moscow jana, Ryabkov alikosoa uamuzi wa Umoja wa Ulaya kuwaondolea waasi wa Syria vikwazo vya silaha, akisema hatua hiyo itadhuru juhudi za amani. Hali kadhalika naibu waziri huyo alitetea mpango wa nchi yake kuiuzia Syria mfumo wa makombora akiuita wenye kuleta utengamano.
Aidha alisema kuwa mkataba wa silaha hizo ulisainiwa kabla ya kuanza kwa vita, kama makubaliano baina ya serikali mbili halali zinazotambuliwa kimataifa.

kutoka  Dw swahili http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: