Spika wa Bunge la Libya ajiuzulu

................... Spika wa bunge la Libya Mohammed al-Megarif amejiuzulu, akiheshimu sheria inayowapiga marufuku watu walioutumikia utawala wa kanali Muamar Gadhafi.
Megarif ambaye alikuwa balozi wakati wa utawala wa Gadhafi kabla ya kujiunga na kambi ya upinzani, alijiuzulu jana, wiki chache baada ya bunge kupitisha sheria inayowakataza maafisa wa serikali ya zamani kushika wadhifa katika ofisi za umma.
Mohammed al- Megarif alijitenga na utawala wa Ghadafi na kukimbilia nje ya nchi mwaka 1980, na alirudi baada ya kuangushwa kwa utawala huo na kuchaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi wa kwanza huru uliofanyika mwaka jana nchini Libya.

chanzo:Dw swahili http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: