UTATA HABARI ZA MWANA MUZIKI SAIDA KUSEMEKANA AMEFARIKI
Kuna tetesi kuwa mwanamuziki mashuhuri Afrika Mashariki, Saida Karoli amefariki dunia
baada ya kuzama maji kufuatia ajali ya boti iliyotokea kwenye ziwa
Victoria. Ajali hiyo ilitokea baada ya boti aliyokuwa akisafiria kutoka
Kisiwa cha Goziba kukumbwa na dhoruba na kuzama katika Ziwa Victoria.
Taarifa hizo zinasema pamoja na Saida Kalori, kuna watu wengine pia wamefariki dunia katika ajali hiyo. Idadi ya waliofariki kwenye ajali hiyo bado haijapatikana
Taarifa hizo zinasema pamoja na Saida Kalori, kuna watu wengine pia wamefariki dunia katika ajali hiyo. Idadi ya waliofariki kwenye ajali hiyo bado haijapatikana
chanzo:Gumzo la jiji
Taarifa: Saida Karoli yuko hai. Kweli ajali ya boti imetokea lakini Saida hakuwemo
3 Comments
Advertisement
Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “…ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria, na kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.”
Nayo Upland FM radio, Kwa kupitia Facebook page yake, imekanusha taarifa za kufariki Saida karoli na kusema msanii huyo ni mzima wa Afya. “TAARIFA: Kumezuka habari zisizo rasmi juu ya mwanamuziki SAIDA KALORI. Tunaomba kuthibitisha kwa Mwanamuziku huyo ni MZIMA wa afya kabisa. Usidanganywe na uzushi wowote. ASANTE.” imesema taarifa hiyo ya Upland FM
chanzo:BlogSy Tanzania