Chama kipya chaanzishwa Afrika Kusini.
Mmoja wa wanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Dr. Ramphele amezindua chama kipya cha kisiasa kutoa changamoto kwa chama tawala cha ANC kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo hapo mwakani.
Dr. Ramphele amewaambia wafuasi wake waliokusanyika wakati wa uzinduzi wa chama hicho mjini Pretoria kuwa ANC haitakiwi kuaminiwa kuinua uchumi wa nchi hiyo.Chama chake kijulikanacho kama Agang chenye maana ya kujenga kimejipanga kupigana na Rushwa na kuimarisha sekta ya elimu kama malnego yao makuu. Dr. Ramphele ni mkurugenzi wa zamani wa Benki ya dunia na ni mke wa zamani wa mpigania uhuru wa Afrika Kusini hayati Steven Biko.
Mchungaji mstaafu Desmond Tutu amemtaja Dr. Ramphele kama mtu hodari na kiongozi mwenye msimamo
chanzo:bbcswahili
0 comments: