LeRoy ajiuzulu kuifundisha DR Congo
Claude LeRoy ameachia ngazi kama mkufunzi wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Kocha huyo kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka
65 alichukua wadhifa huo wa kuifundisha timu ya Leoards kwa mara ya pili
mwezi Septemba mwaka 2011."niliwambia wachezaji wangu kwamba nitaachia ngazi baada ya miaka miwili,"alisema Le Roy,ambaye mechi yake ya mwisho ilichezwa jumapili iliyopita dhidi ya Cameroon.Timu mbili zilitoka sare ya bila kufungana,katika mechi za mchujo wa kutafuta tiketi ya fainali za kombe la dunia.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DR Congo haitafuzu katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 na kama ilivyotarajiwa Timu ya taifa ya Cameroon ilipewa alama tatu baada ya Togo kukiri kwamba mapema mwezi huu ilimtumia mchezaji ambaye hakuruhusiwa kucheza.
LeRoy alisaidia Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kufuzu kwenye fainali za kombe la mataifa ya bara la Afrika mwaka 2013 nchini Afrika kusini,lakini ikashindwa kuvuka hatua ya makundi licha ya kutopoteza mechi hata moja.
Ni kwa mara ya saba LeRoy akisaidia timu kufuzu kwenye fainali za kombe la Afrika baada mafanikio yake akiifundisha Cameroon na kunyakua kombe hilo mwaka 1988.Pia alizifundisha Senegal na Ghana
chanzo:bbcswahili
0 comments: