Dola milioni 7 kwa mwenye habari kuhusu Boko Haram
Marekani inaahidi kutoa zawadi
ya fedha kwa yeyote atakayetoa habari kuhusu makundi ya wapiganaji wa
kiisilamu Kaskazini na Magharibi mwa Afrika.
Wizara ya mambo ya ndani nchini Marekani inasema
itatoa dola milioni saba kwa yeyote atakayetoa taarifa kuhusu aliko
kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau.Yeyote atakayepasha habari kuhusu kiongozi wa zamani wa kigaidi Mokhtar Belmokhtar ataweza kupokea dola milioni tano.
Kundi lake la wapiganaji lijulikanalo kama, Blood Battalion,linasemekana lilifanya shambulizi dhidi ya kiwanda cha gesi, Kusini mashariki mwa Algeria mwezi Januari ambapo mateka 37 waliuawa wakiwemo wamarekani watatu.
Donge nono la dola milioni tano pia lilitolewa kwa mtu ambaye angetoa habari kumhusu kamanda mkuu wa wapiganaji wa kiisilamu Yahya Abu el Hammam, ambaye Marekani ilipanga kushambulia watu na kuwateka nyara wageni katika kanda ya Afrika Magharibi.
Wizara hiyo ilisema kuwa takriban dola milioni 3 zitatolewa kwa watakaotoa habari kuhusu viongozi wengine wa kigaidi wakiwemo, Malik Abou Abdelkarim na msemaji wa kundi la (Mujao) Oumar Ould Hamaha.
Inaarifiwa kuwa Oumar Ould Hamaha, alihusika na visa vya utekaji nyara wa raia wa kigeni nchini Niger mwaka 2008 na kudai kulipwa kabla ya kuwaachilia
Kundi la Boko Haram, limekuwa likifanya mashambulizi makali Kaskazini mwa Nigeria, na kusababisha vifo vya watu 2,000 tangu mwaka 2009.
Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kuwepo uhusiano kati ya Boko Haramna makundi mengine ya kigaidi katika nchi zingine katika kanda hiyo ikiwemo kundi la
AQIM.
Na bbcswahili
0 comments: